BAADA ya Kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Baraza la Vyama na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA kwa kipindi cha miaka 4 ijayo, Rais wa TFF Wallace Karia ameahidi kuimarisha na kuboresha michezo ndani ya nchi wanachama.

Hayo ameyasema baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo nyeti, akisaidiana na Karia amechaguliwa katika nafasi hiyo Makamu wa Rais wawili ambao ni Francis Amin kutoka Sudan ya Kusini na Esayas Jiro wa Ethiopia.

Mkutano Mkuu wa CECAFA uliofanyika nchini Uganda leo na Karia kuwania nafasi hiyo.

Rais wa TFF amezungumza baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo pamoja na vitu atakavyovifanya kwenye nafasi yake, ambapo amesema atasimamia vizuri katika upatikanaji wa wadhamini, kuimarisha michuano ya soka la ufukweni pamoja na kusimamia nchi wanachama na waalikwa wanashiriki kikamilifu kwenye michuano inayoadaliwa na baraza hilo.

Pia katika mkutano huo imeshuhudiwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA, Nicholas Musonye akiachia ngazi katika nafasi yake hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka 20.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...