Muonekano wa gati mpya iliyopo katika Bandari ya Sibwesa iliyopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma ambayo imejengwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) ikiwa ni mkakati wa kuboresha miundombinu ya bandari za Ziwa Tanganyika
Sehemu ya mawe ambayo yamekuwa yakitumika katika ujenzi wa miundombinu ya bandari ya Lagosa
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama akielezea ujenzi wa miundombinu katika bandari za Ziwa Tanganyika ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia bandari ya Sibwesa na Bandari ya Lagosa zilizopo wilayani Uvinza mkoani Kigoma.
 Muonekano wa baadhi ya majengo pamoja gati ambayo imejengwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika bandari ya Sibwesa wilayani Uvinza.
 Sehemu ya muonekano wa gati iliyojengwa katika bandari ya Lagosa wilayani Uvinza mkoani Kigoma 



Na Said Mwishehe-Michuzi TV-Kigoma 

MENEJA wa Bandari za Ziwa Tanganyika Percival Salama amesema kuwa katika Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) inatekeleza miradi miwili ya uboreshaji wa miundombiu ya bandari ikiwemo ya kujenga gati kwenye eneo la Lagosi na kwamba utekelezaji wake umefikia asilimia 85. 

Akizungumza mbele ya waaandishi wa habari, Salama amesema kuwa mradi huo ni wa miezi 24 na hivyo mkandari aliyepewa kazi ya ujenzi wa gati hiyo atatakiwa kukabidhi mradi Aprili 2020.Kwa hiyo utaona ni kwamba mwekelekeo wa mradi huo ni mzuri na utamalizika kwa wakati. 

Amesema mbali ya ujenzi wa gati katia bandari hiyo pia kuna ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mizigo, jengo la abiria, nyumba ya mfanyakazi wa Bandari ambaye atakuwa anahudumia eneo hilo pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine wezeshi ambayo itachangia kufanya shughuli za kibandari kuwa bora na za kiwango kinachohitajika. 

Amefafanua wakati hayo yakiendelea katika Ziwa Tanganyika, pia watawezesha kumairika kwa mawasiliano ya kibiashara kati ya wenzao wa DRC na nchi nyingine ambazo ni jirani na Tanzania.Pia ujenzi wa miundombinu utapunguza gharama kwa wananchi ambao wanasafiri kupitia Ziwa Tanganyika. 

Salama amesema pia kuna mradi mwingine mkubwa ambao unafanyika kwenye Bandari ya Kalya ambayo wao wanaiita Sibwesa ambapo ujenzi wa bandari kubwa tayari umekamilika kwa asilimia 100." Nasi TPA tumeshaweka mashine pale ya kuanza kutoa huduma tafsiri yake tunawaambia wana Kigoma ya kwamba sasa Sibwesa imeanza kutoka huduma na imekamilika na meli zinaweza kutia nanga pale. 

"Kwa hiyo kwenye Mkoa wa Kigoma miradi ya kimkakati utaniona miradi karibu saba infanyika ambayo sasa inakwenda kubadilisha aina ya huduma kwenye Mkoa wa Kigoma,"amesema Salama na kuongeza kuwa kwa mikakati ambayo wameiweka katika kuboresha huduma za kibandari ndani ya Ziwa Tanganyika, uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla unakwenda kuongezeka. 

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwa kuna kuwa TPA dhamira yake ni kuendelea kutoa huduma bora za bandari kwa wananchi na hivyo wamemua kuweka kipaumbele cha kuhakikisha kunakuwa na miundombinu ya uhakika, na kutoa rai kwa jamii inayozunguka maeneo hayo kuzitumia bandari hizo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...