Na Dan Mwambene, Ofisi ya DC Ileje
Wakati Siku ya Walemavu Duniani imeadhimishwa Mkuu wa Wilaya ya Ileje amemtembelea na kumkabidhi baiskeli ya tairi tatu kijana aliyekatwa miguu yote baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Waswahili husema,kabla hufajafa,hujaumbika usemi huu unamwangukia kijana mwenye umri mchanga akiwa na ndoto zenye kumfikisha mbali kimaisha ambazo sasa zimepunguzwa kasi na ulemavu huo.
Akiwa mwenye umri wa miaka 23 mtoto wa nne kati ya watoto saba wa Mzee Odeni Mwambene kijana Costa Mwambene mkazi wa Kitongoji cha Ipapa Kijiji cha Isongole Ileje ameshapoteza miguu yote na kuwa tegemezi.
“Nimeugua kwa karibu miaka mitatu kilianza kijipu kidogo mguu wa kulia na badaye mguu wa kushoto hali iliyomsababishia vidonda na kupelekea nikatwe miguu yote miwili”alisema kijana huyo akiuguza majeraha muda wote kitandani.
Baada ya kupokea ombi la mlemavu huyo hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndg.Joseph Mkude alifika nyumbani kwa wazazi wa Costa na kukabidhi baiskeli ya tairi tatu itakayomsaidia.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi baiskeli hiyo kiongozi huyo aliitaka jamii kutambua kuwa kila mmoja anaweza kuwa mlemavu akashukuru watu walioweza kutoa michango yao wakati wa kumhudumia kijana Costa aliyeanza kuugua mwanzoni mwa mwaka 2017. 
Mdogo wa mlemavu huyo alisema kuwa kutokana na maradhi hayo mke wa kaka yake alishaondoka baada ya kumwuguza miaka miwili tu.
‘’Mwanzo aliomba kwenda kwao kupumzika,lakini katikati ya mwaka huu tukiwa Hospitali ya Ikonda mkoani Njombe alikokatwa miguu tulipigiwa simu na mama yetu kuwa amechukua talaka”alisema kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa wametumia fedha nyingi ikiwemo kuuza nyumba ya mgonjwa,kuuza ng’ombe wanne wa familia wakihangaika kuponya maradhi ya ndugu yao wakitibiwa katika hospitali za Ileje,Kyela,Chitipa-Malawi  na Ikonda Njombe.
Alisema kwa sasa mipango ya maendeleo ya kifamilia imesimama kutokana hali inayowasibu kwani kila baada ya siku mbili hulazimika kukodi gari kwa elfu saba ili kwenda kuhudumiwa Hospitali ya Wilaya umbali wa kilometa saba.  
 kijana Costa Mwambene enzi hizo kabla hajapata ulemavu wa kukatwa miguu yote.

 kijana Costa Mwambene enzi hizo kabla hajapata ulemavu wa kukatwa miguu yote.

DC Joseph Mkude (kushoto)akiwa na Costa Mwambene siku alipomtembelea na kumkabidhi baiskeli ya tairi tatu. 
Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.

Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.

 Kijana Costa Mwambene baada ya kupata ulemavu.
DC Joseph Mkude wa Ileje (aliyevaa shati la bluu) akizungumza mara baada ya kumwona na kukabidhi baiskeli kwa wazazi wa mlemavu Costa Mwambene. 

 Mzee Odeni Mwambene na mkewe Luhobokelo Nyondo wakazi wa Isongole Ileje(kulia) wakimshukuru DC wa Ileje aliyefika nyumbani  kwao kumwona kijana wao mlemavu na kumkabidhi baiskeli ya taili tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...