Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Saitole Laizer akiongea na waratibu wa  mfumo wa taarifa,na ufuatiliaji wa huduma za afya kutoka mikoa na halmashauri nchini
 Picha ya pamoja ya watumishi kutoka wizara ya afya na OR-TAMISEMI na mgeni rasmi
 Waratibu wa mfumo wa taarifa wa ufuatiliaji wa huduma za afya wakiwa kwenye makundi wakiandaa mpango kabambe wa utekelezaji
 Kaimu mkurugenzi msaidizi ufuatiliaji na tathimini kutoka wizara ya afya Tumainiel Macha  akiongea kwenye kikao kazi hicho

 Mwenyekiti wa waratibu hao Dkt. Ally Msoke akitoa neno la shukrani wakati wa ifunguzi wa mkutano huo
Waratibu hao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)  wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho.kinachofanyika chuo cha mipango Dodoma

************************************
Na. Catherine Sungura, Dodoma 

Waratibu wa Mfumo wa Taarifa za Utoaji wa Huduma za Afya (MTUHA) nchi wametakiwa kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za sekta ya afya katika maeneo yao ya kazi. 

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali ambaye pia ni mkurugenzi wa mafunzo na rasiliamali watu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Saitole Laizer wakati akifungua kikao kazi cha waratibu MTUHA wa mikoa na halmashauri Tanzania kinachofanyika jijina hapa. 

Dkt. Saitole amesema kuwa Wizara imeboresha mfumo wa takwimu kulingana na mahitaji ya sasa na zinaingizwa na kuchanganuliwa kwa kutumia program maalum ya kompyuta katika ngazi ya wilaya ijulikanayo kama ‘District health information software-DHIS 2’, hivyo ana imani watasimamia na kuratibu kwa umakini. 

“Matarajio ya wizara ni kuwa takwimu zinazopatikana kutoka katika program hii zitakuwa sahihi na mtatengeneza orodha ya kielekroniki ya vituo vya kutolea huduma za afya ili kusaidia katika mipango na kutoa maamuzi katika Sekta ya Afya”. 

Vile vile Dkt. Saitole aliwataka waratibu hao kuweka mipango kabambe ili kuhakikisha mrejesho wa zoezi la uhakiki wa ubora wa takwimu za afya uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali pamoja na kutoa mafunzo ya mrejesho katika meza maalum zitakazoandaliwa ili kutoa msaada wa watumishi ambao wanahitaji kujifunza,kupata ufafanuzi au kuuliza na kupata majibu ya masuala ya MTUHA yanayowasumbua katika maeneo ya kazi . 

Hata hivyo aliwataka waratibu hao kuhakikisha halmashauri zinatenga fedha kwa ajili ya MTUHA katika mpango kabambe wa halmashauri(CCHP) na timu za za afya za mikoa na halmashauri na Wadau wa Maendeleo wanashiriki kikamilifu katika kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi za Sekta ya Afya. 

Mfumo wa taarifa za utoaji wa huduma za afya nchini umesaidia kuwezesha sekta ya afya kupata takwimu sahihi na kwa wakati zinazowezesha kufanya maamuzi sahihi katika kupanga na kutekeleza malengo yake ili hatimaye kufikisha huduma bora kwa wananchi kutoka asilimia 43 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...