Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuashirika kuzindua Bodi ya Pili ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru leo mkoani Arusha kushoto ni Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii Dkt. John Jingu na Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Rose Mwaipopo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Rose Mwaipopo mara baada ya kuzindua Bodi ya Taasisi hiyo leo mkoani Arusha.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikabidhi vifaa vya kazi kwa Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Bakari George mara baada ya kuzindua Bodi ya Taasisi hiyo leo mkoani Arusha.







Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Pili ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru leo mkoani Arusha mara baada ya kuizindua Bodi hiyo.



Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jmaii Dkt. John Jingu akieleza chimbuko la Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kabla ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo mkoani Arusha.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitazama kitabu katika Mkataba ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kabla ya kuzindua Bodi ya Pili ya Uendeshaji wa Taasisi hiyo leo mkoani Arusha.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa cheti na zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jmaii Tengeru aliyefanya vizuri katika masomo kabla ya kuzindua Bodi ya Pili ya Uendeshaji wa Taasisi hiyo leo mkoani Arusha.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa kutoka kwa wanafunzi wa Taasisi ya Maendeleo ya Jmaii Tengeru kabla ya kuzindua Bodi ya Pili ya Uendeshaji wa Taasisi hiyo leo mkoani Arusha.


Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya pili ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (hayupo pichani) wakati akizindua Bodi hiyo leo mkoani Arusha.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru mara baada ya kuzindua Bodi ya Taasisi hiyo leo mkoani Arusha wa pili kulia waliokaa ni Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu na wa pili kushoto walioakaa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Rose Mwaipopo.



Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

………………..

Na Mwandishi Wetu Arusha

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameizindua Bodi ya pili ya uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na kuitaka kuleta chachu ya mabadiliko katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii nchini.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mkoani Arusha wakati akizungumza na wajumbe wa Bodi hiyo ambayo ina jukumu ya kuratibu na kusimamaia shughuli zinazofanyawa na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru.

Waziri Ummy amewataka wajumbe wa Bodi hiyo kuisaidia Serikali katika kuhakikisha Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru inaleta matokeo chanya kwa jamii hasa inayowazunguka na kuhakikisha itakuwa kituo cha mfano cha Taaluma ya Kada ya Maendeleo ya Jamii nchini.

Ameitaka Taasisi hiyo kuzingatia mafunzo kwa vitendo kwa kuongeza uhusiano mzuri kati ya nadharia na vitendo katika mitala iliyopo na kuweka mkazo katika kuhakikisha mafunzo wanayoyatoa yanawasaidia wahitimu kuwa na nandhari ya kujiajiri zaidi kuliko kuajiriwa.

Pia ameitaka Bodi hiyo kuweka mkazo katika kutatua changamoto za ajira kwa kuhakikisha inawapa wanafunzi stadi za kuwawezesha kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine kupitia fani walizosoma hasa fani ya Maendeelo ya Jamii.

“Niwatake mjenge ushirikiano kati ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na Taasisi zingine ili wahitimu waweze kujitolea na wengine kuweza kupata ajira katika Taasisi hizo hasa Mashriika Yasiyo ya Kiserikali” alisema Waziri Ummy

Waziri Ummy ameongeza kuwa Taasisi hiyo ina umuhimu katika jamii hivyo kuitaka kutoa mchango katika jamii katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii inayoizunguka Taasisi hiyo ili kupata jawabu za changamoto hizo.

Aidha Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru kuhakikisha wanachangia katika mfuko wa Serikali kwa kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kila Taasisi ya Serikali kuchangia katika mfuko wa Serikali ndani ya siku 60.

“Agizo hili msije mkasema sisi hatuzalishi faida mnatakiwa kutoa mchango wenu kama Taasisi ya Serikali katika mfuko wa Serikali ambao ni muhimu kwani ndio unasaidia kutoa huduma muhimu kwa wananchi” alisema Waziri Ummy

Kwa upande wake Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa Bodi iliyopita iliweza kuandaa programu mbalimbali za mafunzo, walifanya maandalizi Sera 13 za usimamizi wa Taasisi mbalimbali waliwezesha kuongozeka kwa udahili wa wanafunzi 276 kwa mwaka wa masomo 2014/2015 mpaka 1204 kwa mwaka 2018/2019 na kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru Dkt. Rose Mwaipopo amesema Bodi hiyo inafanya majukumu yake kwa mujibu wa Sheria na kuzingatia umuhimu wa kada ya Maendeleo ya Jamii katika kuchochea maendeleo ya nchi.

“Tunatazamia kuleta chachu katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii hasa katika kuleta mapinduzi ya kifkra kwa wananchi katika kujiletea maendeleo yao wenyewe” alisema Dkt. Rose.

Bodi ya pili ya Uendeshaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru imezinduliwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Rose Mwaipopo na itahudumu kwa muda wa miaka mitatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...