NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO.

Yahya Yasini (34)Mkazi wa kitongoji cha Miembeni kijiji cha Mandela kata ya Likuyuseka Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma alinusurika kuliwa na mamba katika mto Lumbegea uingizao maji yake katika mto Luegu uliopo katika kijiji hicho.

Akiongea akiwa katika kituo cha afya Namtumbo bwana yahaya alisema kuwa ni mapenzi yake mola ndiye aliyemsaidia kupata nguvu ya kushinda pambano kati yake na huyo mamba na kumwachia asimgeuze kitoweo.

Alisema alikuwa anavuka mto Lumbegea akitokea kitongoji cha Miembeni kwenda ofisi za kijiji chao cha Mandela na alipokuwa anavuka mto huo alikamatwa na mamba huyo na kupambana naye mpaka alipomwachia.

Kwa mujibu wa wananchi wa kitongoji cha Miembeni ambao wanamfahamu vizuri bwana yahya hawakutaka majina yao yatajwe walidai bwana yahya ni mtegaji wa midema ya kunasia samaki hivyo inawezekana kabisa alikuwa katika zoezi la kwenda kuangalia midema aliyokuwa ameitega na kukutana na mamba huyo.

Wananchi hao walidai mamba katika mto Lumbegea hutokea katika mto Luegu wakikimbia maji mengi katika mto Luegu lakini hukaa katika mabwawa yenye maji mengi katika mto huo wa Lumbegea hivyo inawezekana alitega mitego iliyosababisha akutane na huyo aliyekimbia maji mengi katika mto luegu na kujificha katika mto Lumbegea walisema wananchi hao.

Pamoja na hayo walidai mamba wakati wa mvua nyingi mto luegu hufurika maji mamba na samaki waliopo katika mto huo huingia katika vijito vinavyoingiza maji yake katika mto huo na kubaki katika vijito mpaka maji yanapopungua katika mto Luegu na baadae hurudi tena.

Mganga mkuu wa kituo cha afya cha Namtumbo bwana Lewanga Mandari alikiri kumpokea Yahya Yasini aliyekuwa na majeraha kwenye mguu wake yaliyosababishwa na kung”atwa na meno ya mamba na kudai kuwa anaendelea kupatiwa matibabu katika kituo hicho cha afya huku afya yake ikiendelea kuimarika siku hadi siku . 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...