Na.WAMJW-Dodoma

Jumla ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi cha julai hadi desemba 2019 kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii

"Katika kipindi hiki matarajio yalikua ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua,hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wajawazito 813,923 sawa na,asilimia 74 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma"Amesema Ummy Mwalimu.

Kwa upande wa wajawazito waliofanya mahudhurio ya kliniki,Waziri huyo amesema kuwa jumla ya wajawazito 797,803 sawa na asilimia 73 ya walengwa walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi kama mwongozo ulivyoelekeza.

Aidha, amesema kuwa asilimia 87.4 ya wajawazito sawa na akinamama 886,810 walipatiwa dawa za kukinga Malaria na jumla ya dozi 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 walipewa dawa ya kuzuia upungufu wa damu(FEFOL).

Hata hivyo Waziri Ummy amesema,kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ilihakikisha dawa muhimu za kuzuia na kutibu kifafa cha mimba na kukinga na kutibu kupoteza damu baada ya kujifungua,kutibu magonjwa na,watoto chini ya miaka mitano uliimarika kwa zaidi ya asilimia 85.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Zainab Chaula akifuatilia taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa wizara yake Mhe.Ummy Mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi.cha julai.hadi.desemba 2019 kwa kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii Mhe. Peter Serukamba akiongea wakati wa kikao hicho

Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Benard Konga akiwasilisha taarifa ya utendaji wa mfuko huo

Waziri Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa kwenye kamati
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi.cha julai.hadi.desemba 2019 kwa kamati ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...