Na Abdullatif Yunus wa Michuzi TV.

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera limewatunuku Vyeti vya Umahiri na Ujasili pamoja na Pesa Taslimu Jumla ya Askari Polisi 19 kutoka katika Vitengo mbalimbali, kufuatia Utendaji kazi wao uliotukuka kwa Mwaka Uliopita 2019.

Tukio hilo limefanyika mapema Januari 08, 2019 katika Viwanja vya Field Force Unit (FFU) Nshambya Manispaa ya Bukoba, kutokana na maelekezo ya Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi katika ziara aliyoifanya Mkoani Kagera Mwezi wa Septemba Mwaka Jana, alipokutana na baadhi ya Askari katika maeneo ya Nyakanazi,  Biharamlo na kuridhishwa na utendaji kazi wao, hivyo kuwatunuku vyeti pamoja na Shilingi Elfu 50 kila mmoja, na baadhi kuwapandisha vyeo wakiwemo Askari kutoka kikosi maalumu cha kupambana na Ujambazi.

Vyeti na Zawadi hizo vimekabidhiwa Rasmi na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti ambae pia amelipongeza Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa jinsi walivyofanikiwa kudhibiti hali ya uhalifu kwa mwaka Jana (2019), Taarifa ikieleza kuwa hakuna tukio lolote lililoripotiwa la uhalifu kwa kutumia silaha (Bunduki), na hivyo kuongeza zawadi ya shilingi Elfu Hamsini  kwa kila mmoja kwa Askari hao waliotunukiwa vyeti hivyo.

Mkoa wa Kagera unapakana na Nchi Jirani NNE, zikiwemo Nchi ambazo zimekuwa zikiripotiwa kwa matukio mbalimbali ya kihalifu kwa kutumia silaha, hata hivyo hali kwa sasa ni shwari kupitia kamati nzima ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, jambo ambalo limeongeza fursa pia kwa wawekezaji kuja kuwekeza Mkoani hapa, kutokana na kuhakikishiwa  Usalama muda wote.
 Pichani Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti, akikabidhi Vyeti pamoja na Pesa Taslimu kwa Askari Polisi waliofanya vizuri Mwaka Jana na kutunukiwa Vyeti hivyo na Inspekta Jenerali Simon Sirro.


Pichani wakionekana Askari katika Gwaride Maalum la Utoaji zawadi na Vyeti Kwa Askari Polisi Mkoani Kagera waliofanya Vizuri katika kazi zao kwa kipindi cha Mwaka Jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...