Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akikagua rangi zinazotengenezwa na kiwanda cha Billion Paints mara baada ya kukabidhiwa ndoo 500 za rangi ambazo zimeelekezwa katika ujenzi wa shule, leo jijini Dar es Salaam.
Meneja masoko wa kampuni ya utengenezaji rangi ya Billion Paints Ruth Muruve akizungumza na waandishi wa habari Mara baada ya kukabidhi rangi hizona kueleza kuwa huo ni mwendelezo wa ushirikiano baina yao na RC Makonda katika kuboresha sekta ya elimu, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza mara baada ya kupokea rangi hizo ambapo amewaomba wadau zaidi kujitokeza katika kuboresha sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Ndoo za rangi zilizotolewa na Kampuni ya utengenezaji rangi ya Billion Paints kwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa kampuni hiyo katika kuboresha sekta ya elimu nchini, leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea ndoo mia tano kutoka katika kampuni ya utengenezaji wa rangi cha Billion Paints ambazo zimeelekezwa katika shule za jijini humo ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho na kukabidhiwa rangi leo, Makonda amesema kuwa kiwanda hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2017 na kijana mtanzania aliyeitikia wito wa Rais Dkt. Magufuli katika suala la ujenzi wa viwanda matunda yameanza kuonekana na wamekuwa sehemu ya ushiriki wa shughuli za kijamii ikiwemo elimu.

Makonda amesema kuwa rangi hizo zitasaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 380 kwa uwiano wa wanafunzi 50 kwa darasa moja unaendelea katika Wilaya ya Temeke ambako wanafunzi 5970 wameshindwa kuanza masomo yao kutokana na ufinyu wa madarasa.

"Wanafunzi 5970 waliofaulu walikosa vyumba vya madarasa na kupitia waraka uliotolewa na Wizara ya elimu tunategemea kufikia Machi Mosi wanafunzi wote watakuwa darasani wakiendelea na masomo, na tunawashukuru Billion Paints kwa mchango huu na kwa kutambua hili tutachora 'Billion' ili kutambua mchango huu" ameeleza.

Aidha Makonda amesema kuwa hadi kufikia sasa shule mpya nne zimeanzishwa, ujenzi wa madarasa na matundu ya choo unaendelea na hiyo ni pamoja na ukarabati wa miundombinu na madawati.

"Ninawaomba wadau na washiriki kama Billion wajitokeze na tushirikiane katika kuimarisha sekta hii adhimu na wazazi hawatachangishwa chochote elimu itatolewa bure kama Rais Dkt. John Joseph Magufuli alivyoelekeza" amesema Makonda.

Vilevile amewashauri vijana kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kujenga taifa imara kama mwanzilishi wa kiwanda hicho alivyothubutu na kuajiri vijana wengine arobaini.

Kwa upande wake Meneja masoko wa kiwanda hicho Ruth Muruve amesema amesema kuwa wataendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kuboresha sekta ya elimu nchini na wametoa rangi hizo ili kutengeneza mazingira bora ya ujifunzaji kwa wanafunzi.

Amesema kuwa kampuni hiyo ya wazawa inazalisha aina saba za rangi na inapatikana kwa gharama nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...