Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema mpango wa vifurushi umekuja kwa ajili ya kuwajumuisha watanzania wote.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akitoa kadi za bima za afya kwa wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya pamoja wanachama waliojiunga kwa mpango wa vifurushi, leo Mkoani Mwanza.
Makamu Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema suala la vifurushi limekuwa kuwa mkombozi kwa machinga.
Makamu Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe  akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya bima ya afya Mkoani Mwanza, ambapo alisema wamelipokea vyema suala la vifurushi vya Bima ya Afya kwani ni muhimu kwa afya zao.PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO
…………………..
Na Mwandishi Wetu.

Jumuiya za Wajasiriamali wadogowadogo na Waendesha Bodaboda nchini wamepongeza hatua ya kuanzishwa kwa vifurushi vya bima ya afya ambavyo vimewawezesha  katika kupata matibabu ya uhakika pindi wanapoumwa.

Wakiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya viongozi wa jumuiya hizo wamesema ilikuwa ni hitaji lao la muda mrefu la kuhakikisha wanachama wao wanakuwa na uhakika wa matibabu kwa kuwa na bima za afya.

“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano kwa kuwa na maono ya kuhakikisha machinga nasisi tunakuwa na uhakika wa matibabu, awali ilikuwa ni ngumu sana unaenda hospitali ukiwa na hofu ya gharama lakini kwa sasa tunatembea kifua mbele, tunapata tiba popote nchini kwa vifurushi hivi”-Stephen Lusinde Mwenyekiti wa Machinga Taifa
Naye Mwenyekiti wa Bodaboda Taifa Bw. Michael Haule amesema kuwa ujio wa mpango huu wa vifurushi ni uthibitisho kwamba serikali ya awamu ya tano kila mtu ni sawa na ndio maana wao kama bodaboda sasa wamewekewa utaratibu rahisi wa kujiunga na vifurushi vya bima ya afya kwa gharama nafuu kabisa.

“Zamani ilikuwa ni ngumu sana kumkuta bodaboda anamiliki kadi ya bima ya afya, bodaboda wengi wawepoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za matibabu kutoka na ajali, ila kwasasa suala hilo ni historia, bodaboda sasa ni kama wafalme tunajidai na kadi zetu”- Michael.

Mwenyekiti wa Bodaboda  Mkoa wa Mwanza Bw. Gerald Nyerembe alisema kuwa wamelipokea suala la vifurushi kwa kuwa ni muhimu kwa afya zao na wanafarijika sana kwa Serikali kuwatambua kwani bima imekuwa na faida kubwa kwao.

Aidha, Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mwanza Bw. Joseph Samwel amesema suala la vifurushi limekuja kuwa mkombozi na kuokoa maisha ya wajasiriamali wadogo kwani bila afya hakuna maendeleo hivyo wajasiriamali hawana budi kuliona suala la vifurushi kama mkombozi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...