Waziri Ummy Mwalimu akiwa kwenye wodi ya wagonjwa walioupandikizaji figo
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kipimo cha uchunguzi wa saratani ya matiti’Mammography’ kilichopo kwenye kwenye hospitali ya Benjamin Mkapa
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwa kwenye chumba cha kipimo cha CT-Scan kwenye hospitali hiyo.
Waziri Ummy Mwalimu akiongea na watumishi wa hospitali hiyo(hawako puchani)
Mmoja wa watoa huduma kwenye idara ya wagonjwa wa dharura akitoa maelezo kwa Waziri wa afya Waziri Ummy akiwa na viongozi wa hospitali hiyo akitembelea maeneo mbali mbali ya utoaji huduma



*******************************

Na. Catherine Sungura-Dodoma

Hospitali ya Benjamin Mkapa imetakiwa kujiunga na tiba mtandao ili kuweza kutoa tiba kwa wagonjwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuwapunguzia wagonjwa muda wa kusubiri majibu hususani ya mionzi .

Rai hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipoitembelea hospitali hiyo kujionea hali ya utoaji huduma.

“Nawaelekeza ni vyema mkajiunga na huduma ya tiba mtandao ili muweze kutoa huduma kwa haraka na kwa ufanisi zaidi, mnatakiwa mkajifunze huduma hii kutoka hospitali ya Muhimbili au MOI”. Amesema waziri Ummy.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa hivi sasa kwenye hospitali nyingi kuna changamoto za wataalam wa kusoma picha kwani wataalam wengi waliopo ni wale wa kupiga ”bahati nzuri sisi tunao wataalam wengi wa kupiga picha mana kwenye mionzi kuna aina mbili za wataalam wapo wa kupiga picha (radiographer) na wa kusoma picha, hivyo serikali itahakikisha inapata wataalam wengi zaidi wa kusoma ili kukidhi mahitaji.

Waziri Ummy amesema wizara ina lengo la kuziunganisha hospitali za wilaya pamoja na vituo vya afya kwenye mfumo wa hospitali za rufaa za mikoa kwa kufunga senta zitakazosaidia hospitali za wilaya na vituo vya afya vinavyofanya vipimo vya ‘utra sound’ na ‘x-ray’ na majibu yakasomwa haraka na wataalam wa Hospitali za rufaa na kutoa majibu haraka bila kumsubirisha mgonjwa kwa muda mrefu.

Alitaja hospitali zilizojiunga na tiba mtandao ni pamoja na hospitali za rufaa za mikoa ya Lindi na Morogoro , pia hospitali teule za wilaya za Nyangao,Turiani na hospitali za wilaya ya Nachingwea,kilosa na Mvomero.

Wakati huo huo Waziri Ummy ameitaka hospitali hiyo kupunguza gharama za kulipia uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake kutoka elfu sabini hadi elfu thelathini kama hospitali zingine za taifa zinavyofanya.

Hata hivyo waziri huyo ametoa wito kwa wananchi wa Dodoma na mikoa jirani kutosafiri hadi dar es salaam kupata huduma za kibingwa kwani huduma zote karibu zinapatikana hapo na hivyo ameahidi wizara wataleta madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu pamoja na mifupa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...