Na Leandra Gabriel, Michuzi TV 

CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA) kampasi ya Dar es Salaam kimewakutanisha walimu wakuu kutoka shule za Sekondari za Serikali kutoka Manispaa ya Kinondoni na zile zilizojirani na Manispaa hiyo na kujadili namna bora ya usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali pamoja na kusimamia manunuzi hitajika kwa ufasaha zaidi.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo iliyofanyika leo katika kampasi ya Chuo hicho iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Patricia Henjewele amesema kuwa jambo hilo lililofanywa na chuo cha IAA ni la kuigwa na taasisi za namna hiyo hasa kwa kuwapa walimu hao ujuzi zaidi juu ya namna bora ya kutumia rasilimali fedha zinazotolewa na Serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

Aidha amehaidi ushirikiano na utatuzi wa changomoto mbalimbali zinazozikabili shule hizo ikiwemo ukosefu wa wahasibu wa shule wenye fani ya uhasibu pamoja na uboreshwaji wa miundombinu ya ujifunzaji.

Pia Meneja wa kampasi hiyo Dkt. Ikandilo Kushika amesema kuwa licha ya tawi hilo kutoa shahada katika ngazi ya shahada za awali, Astashahada na shahada za uzamili bado wameona kuna haja ya kutoa mafunzo ya uongozi pamoja na kujadili namna bora ya kusimamia mapato, matumizi na kutoa ripoti na hiyo ni sambamba na usimamizi wa rasilimali zilizopo kwa uhakika.

Amesema kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwapika wataalamu wenye tija na mwezi Machi mwaka huu dirisha kwa ngazi za shahada za awali, Astashahada na shahada za uzamili litafunguliwa katika kampasi hiyo na ameahidi kuendelea kushirikiana na shule za sekondari ili kuendelea kuwapika wataalamu ambao watashiriki katika ujenzi wa taifa ipasavyo.

Vilevile mhadhiri mshauri na mtafiti katika fedha na uhasibu Dkt. Erick Mwambuli akifafanua namna bora ya usimamizi wa rasilimali fedha zinazotolewa na Serikali katika shule, amesema kuwa walimu wakuu wanajukumu la Kuhakikisha na kuangaalia namna rasilimali hizo zinavyotutumika na hiyo ni pamoja na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya fedha hali itakayojenga heshima, uaminifu pamoja na matumizi sahihi ya rasilimali.

Dkt. Mwambuli amesema kuwa walimu ni chachu katika kuwajenga wanafunzi ili waweze kufanya vizuri zaidi katika masomo yao na hiyo itafanikiwa ikiwa rasilimali zilizopo zitatumiwa ipasavyo katika kujenga na kuendeleza sekta ya elimu nchini.

Baadhi ya walimu wameeleza changamoto inayowakumba zaidi ni uhaba wa fedha, kukosekana kwa wahasibu wenye fani katika Sekondari za kata pamoja na gharama kubwa za vifaa vya shule ambapo wameishauri Serikali kurudisha bohari ambazo zilikuwa na gharama ya chini ya vitendea kazi; na hiyo ni pamoja na wakurugenzi kubeba jukumu la walinzi wa shule kama waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim alivyoelekeza.
 Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Patrisia Henjewele akizungumza katika warsha hiyo ambapo amekipongeza Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)  kampasi ya Dar es Salaam  na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto , leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Meneja  wa Chuo Cha Uhasibu Arusha (IAA)  kampasi ya Dar es Salaam Dkt.Ikandilo Kushoka akizungumza katika warsha ya uongozi na mafunzo ya usimamizi wa fedha kwa walimu wa shule za sekondari za Serikali ambapo amesema kuwa wanaamini baada ya warsha hiyo rasilimali zilizopo hasa Fedha zitatumika zaidi katika kujenga sekta ya elimu, leo jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri mshauri na mtafiti katika fedha na uhasibu Dkt. Erick Mwambuli akitoa somo katika warsha hiyo ya uongozi na usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali kwa walimu wa shule za Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni ambapo amewashauri walimu wakuu kushiriki katika mpango faafu wa matumizi ya rasilimali hizo, leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya walimu wakifuatlia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa katika warsha hiyo ya masuala ya uongozi na usimamizi wa fedha kwa walimu wa shule za sekondari za Serikali kutoka Manispaa ya Kinondoni,leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Patrisia Henjewele akikadhi vyeti kwa Baadhi ya walimu walio shiriki arsha hiyo ya uongozi na usimamizi wa fedha zinazotolewa na Serikali kwa walimu wa shule za Sekondari wa Manispaa ya Kinondoni,leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...