`WAZIRI wa Wizara ya Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mussa Azzan Zungu amesema kuwa mitumba ni sehemu ya mazingira na nisehemu ambayo inachafua mazingira na kuharibu hadhi ya nchi yetu.

Hayo ameyasema leo mara  baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema  vitu vingine lazima tuanze kubadilika.

Aidha, Zungu amesema wizara anayoiongoza ni ngumu na kuna changamoto nyingi katika wizara, katika utendaji wa baraza la mazingira NEMC na kwenye nguvu kazi ya baraza la mazingira NEMC.

"Mheshimiwa Rais, umepiga vita mifuko ya plastiki umefanikiwa sana.Mheshimiwa Rais hongera sana lakini mifuko hii sasa inarudi kwa njia za pembeni,"amesema  Zungu.

Amesema kuwa watu wanatumia vifungashio (Carrier bags) zimebadilishwa matumizi na kutumika kinyume na kanuni za utaratibu zilizowekwa na Serikali na Waziri aliyepita.

Aidha Zungu amehoji kwa Baraza la Mazingira NEMC, kwanini vitu visivyo na hadhi bado vinakuwepo nchini, na kwanini vitu hivi badi vinapita kwenye mipaka na kwanini vitu ambavyo havina nembo vinakuwepo mtaani wakati kanuni na sheria zipo.

Wakati huo huo amemuahidi Rais Dk.Magufuli, kudhibiti na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kwa vizazi vya sasa na vizazi vya kesho na vizazi vijavyo.Pia Zungu amewaomba wawekezaji ambao wametimiza masharti na vigezo vya kisheria waende wakaonane na mamlaka zinazohusika wapate vibali.
 
 "Tusiwe kikwazo cha kuzuia wawekezaji kuendeleza viwanda na kuifanya Tanzania kuwa ni nchi yenye uchumi wa kati."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...