Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst),
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akiagana na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bw. Mohamed Hamad baada ya kikao na
Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kilichofanyika
ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo. Kikao hicho kilikuwa na lengo
la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya
utawala bora.
Baadhi ya Makamishna na Viongozi
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wakimsikiliza Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao
kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kuzungumzia namna
ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi. Fatuma Muya akitoa maoni yake
wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H.
Mkuchika (Mb) na Makamishna wa Tume hiyo kilichofanyika ofisini kwake
Mtumba, jijini Dodoma leo kilichokuwa na lengo la kujadiliana namna ya
kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst),
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumzia namna ya kufanya kazi kwa
ushirikiano katika masuala ya utawala bora na Makamishna wa Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora waliomtembelea ofisini kwake Mtumba, jijini
Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst),
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) (wa tatu kutoka kushoto mstari wa mbele)
akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi na Utawala Bora mara baada ya kikao kilichofanyika ofisini
kwake Mtumba, jijini Dodoma leo kilichokuwa na lengo la kujadiliana
namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano katika masuala ya utawala bora.
****************************
Na Happiness Shayo – Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amekutana na Makamishna wa Tume yaHaki za Binadamu na Utawala Bora kwa lengo la kujadiliana namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano hasa katika masuala ya utawala bora ili kuboresha utendaji kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao kazi hicho kilichofanyika ofisini kwake Mtumba, jijini Dodoma leo, Mhe. Mkuchika amesema ofisi yake iko tayari kushirikiana na Tume hiyokwani ni wajibu na pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa akisisitiza kushirikiana kwa pamoja kabla ya kupeleka hojamezani kwake.
Aidha, Mhe. Mkuchika amesema kuwa idadi ya malalamiko ya wananchi yanayofanyiwa kazi na ofisi yake yanaongezeka kila mwaka kutokana na utandawazi, kuwapo kwa uwazi serikalini na kutolewa kwa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kudai haki zao za msingi.
Mhe. Mkuchika ameweka bayana kuwa ofisi yake inashughulikia masuala ya utawala bora katika sekta zote hivyo malalamiko yote akitolea mfano wa sekta ya maji, madini n.k. yamekuwa yakiwasilishwa ofisini kwake.
Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu za Utawala Bora, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuomba ushirikiano wa utendaji kazikati ya ofisi yake na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa sababu kwa pamoja ofisi hizo zinashughulikia masuala ya utawala bora.
Akizungumzia majukumu ya Tume hiyo, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu amesema kuwa, ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko katika eneo la haki za binadamu, ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na malalamiko yanayohusu sekta nyinginezo kutoka kwa wananchi, hivyo imekuwa ikiwasaidia walalamikaji kutatua changamotozinazowakabili kwa kuwasiliana na taasisi husika.
Jaji (Mst.) Mathew amesema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali inazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake, ofisi yake itaendelea kufanya kazi kwabidii na kuhakikisha kunakuwa na matokeo chanya katika kuwahudumia wananchi.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamishna wa Tume ya Haki za Binadamu za Utawala Bora na baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma naUtawala Bora, ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na kuboresha utendaji kazi wa ofisi hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...