Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Manyara na kuwasisitiza kujisajili kama ilivyoutaratibu wa kisheria alipofanya kikao na wadau hao leo, kwa lengo la fahamu changamoto zao na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo.
Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo akiwaeleza wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Manyara (hawapo pichani) mikakati ya serikali ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu ambapo kwa sasa imeanza kutumika mifumo ya kidigitali kama SwahiliFlix na Netflix katika kikao kilichofanyika leo Mjini Babati katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza na wakwanza kushoto ni Katibu Tawala Babati Bw.Halfani Matipula.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na mmoja ya wasanii wa filamu wa Mkoa wa Manyara Bw.Mtanga Mdee (kulia) alipomkabidhi CD ya moja ya kazi yake ya filamu aliyofanya na iko sokoni,katika kikao chake na wadau hao leo Mjini Babati,wa pili kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo.
Wasanii wa kikundi cha Kwaraa Family kutoka Babati Mjini Kata ya Majengo Mapya wakionyesha igizo lao mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (hayupo pichani) leo wakati wa kikao cha wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Manyara aliyebeba kipaza sauti ni Bi.Fatna Hussein,na kijana aliyebeba kipaza sauti ni Isack.
******************************
Na Anitha Jonas – WHUSM,Babati
Manyara.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amewataka wasanii wanajisajili kama ilivyoutaratibu ilikuendesha shughuli za usanii katika mfumo rasmi na msanii anaweza kujisajili katika Halmashauri yake kupitia Afisa Utamaduni bila kwenda Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Mkoani Manyara katika Wilaya ya Babati Mjini alipofanya kikao na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kufahamu kero zao na kuweza kujibu hoja mbalimbali pamoja na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo.

“Serikali inajipanga kuanzisha Kanzi Data ya wasanii wa tasnia mbalimbali nchini hivyo basi ni vyema mkajisajili , kumekuwa na changamoto ya kujua wanatasnia wa filamu wangapi wanafanya kazi kama Uandaaji wa Filamu,Uongozaji wa Filamu na Uandaaji wa Miswada ya Filamu kwani zipo fursa mbalimbali zinajitokeza lakini namna ya kuwafikishia wadau hao inakuwa changamoto,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Mhe.Shonza pia aliwasihi wasanii vijana wa mkoa huo kujiunga katika vikundi na kwenda katika Halmashauri zao kuchukua mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kujikwamua kiuchumi hiyo nifursa kwao na wasiiache ipote sababu serikali inajali vijana hivyo waache kulalamika na kuomba kusaidiwa kwani mikopo hiyo ipo na haina riba.

Pamoja na hayo na Kaimu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo aliwaeleza wasanii hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo kwa kuwaeleza kuwa tayari wameanza utaratibu wa kuimarisha mfumo wa usambazaji wa kazi za filamu kwa kuhamia mfumo wa digitali ambapo filamu zinaanza kuangaliwa katika kumbi za sinema na zoezi la kuziweka katika CD na DVD ni hatua ya mwisho ambapo msanii anakuwa ameshapata faida yake.

“Bodi imeendelea kutangaza fursa kwa wadau mbalimbali watakao ungana na wasanii watanzania kufanya nao filamu zenye ubora na tayari nchi mbalimbali zimejitokeza ikiwemo Namibia pia wasambazaji wa mfumo wa kidigitali kama Swahiliflix na Netflix lengo ni kuhakikisha tasnia inakuwa na tunakomesha uharamia wa kazi za filamu na wasanii wananufaika na kazi zao,”alisema Dkt.Kiango.

Hata hivyo nae Afisa Utamaduni Mkoa wa Manyara Bi.Frida Nkarange aliwasisitiza wadau hao wa tasnia ya filamu kuhakikisha wanakuwa karibu na maafisa utamaduni wa maeneo yao ili waweze kuwapa ushauri na kuhakikisha wanaudhuria vikao vinavyowahusu kwani vinamanufaa kwa kazi zao.

Halikadhalika Katibu wa Chama cha Wasanii Mkoa wa Manyara Bw.Dulla ambaye ni msanii wa muziki aliwasisitiza wasanii wenzake kujituma na kuandaa kazi nzuri zilizozingatia ubora kwani hizo ndiyo zitakazo watangaza na kuwapa heshima badala ya kulalamika kuwa wanadharauliwa kwani msanii mwenye kazi nzuri lazma ataheshimika .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...