Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IRAN imekua ikikumbwa  na matukio kadhaa yahusuyo kuanguka kwa ndege na leo ndege ya Iran iliyokuwa na abiria 136  imeteleza katika barabara ya uwanja  wa ndege ilipokuwa ikitua huku picha zikionesha baadhi ya abiria wakiwa wamepata majeraha madogo.

Imeelezwa kuwa ndege hiyo mali ya kampuni ya Caspian matairi yake hayakujimudu wakati ilipokuwa tayari kutua.

Maafisa nchini humo imeeleza kuwa rubani alikuwa makini na aliishusha ndege hiyo haraka na kujikuta katika barabara huku maafisa wa afya wakisema kuwa abiriwa wamepata na majeraha madogo miguuni.
Picha zimeonesha matairi ya ndege hiyo yakiwa yameharibika na huenda ndege hiyo iliteleza bila matairi.

Licha ya kusema kuwa uchunguzi bado unaendelea msemaji wa shirika la safari za anga Jafarzadeh Reza ameeleza kuwa leo alfajiri ndege hiyo iliteleza kutoka katika barabara yake na hakuna kifo kilichopatikana 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...