Na Karama Kenyunko

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imevifutia hati za usajili wa vyuo vikuu vitano, kikiwemo Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba  na Teknolojia (IMTU ) Vituo vya  vyuo vikuu vitatu na Chuo Kikuu kishiriki kimoja kutokana kushindwa kuboresha  mazingira ya kujifunzia na kufundishia huku vyuo  vingine wamiliki  waliomba  kusitisha utoaji wa Mafunzo.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 21,2020 Katibu Mtendaji wa TCU, Prof.Charles Kihampa amesema kati ya mwezi Oktoba 2016 na Januari 2017 Tume imefanya ukaguzi maalum wa kitaaluma kwa taasisi 64 za vyuo vikuu ,Vyuo vikuu vishiriki na vituo vya vyuo vikuu lengo ikiwa kuhakikisha kuwa elimu ya juu itolewayo inakidhi viwango vya ubora kitaifa, ,kikanda na kimataifa.

Amesema, matokeo ya ukaguzi yalibainisha kasoro mbalimbali katika uendeshaji wa vyuo vikuu nchini ambapo vyuo 45 vilikutwa na kasoro ndogondogo huku vyuo 19 vilikutwa na makosa makubwa ambapo miongoni mwa vyuo hivyo vilivyofutiwa hati  za usajili ni pamoja na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira(JOKUCo),Chuo Kikuu cha Mlima Meru(MMU), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba  na Teknolojia (IMTU ) na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB).

Alisema Chuo Kikuu kishiriki cha Askofu Mkuu Yakobo(AJUCo),na Chuo Kikuu kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugamba (CARUMUCo) wamiliki wake waliomba kusitishiwa utoaji wa mafunzo huku vituo vilivyoomba kusitishiwa kutoa mafunzo ni  kituo cha Chuo Kikuu cha Teofilo cha Dar es Salaam cha Teku,Kituo cha Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania(Mtakatifu Marks )na kituo cha Chuo kikuu cha Jomo Kenyatta cha Kilimo na Teknolojia cha Arusha .

Amesema uchunguzi wao umebaini kuwa baadhi ya vyuo havina uwezo wa kujiendesha hata kama vikipewa muda zaidi hivyo TCU katika vikao vya mbali mbali vilivyofanyika kati ya mwezi Agosti 2019 na Januari 2020 imeamua kufuta hati za vyuo hivyo baada ya mashauriano na maombi yaliyofanywa na wamiliki wa vyuo vikuu vishiriki  na Vituo vya Vyuo Vikuu kusitisha utoaji wa mafunzo hayo katika kikao cha TCU.

Hata hivo, Prof.Kihampa amesema hakuna wanafunzi walioathiriwa na zoezi hilo kwa kuwa wanafunzi walikuwa tayari wameshabadilishiwa vyuo vingine na wengine wameshamaliza masomo yao tangu  Oktoba mwaka jana.

Alisema Tume imejiridhisha na maboresho yaliyofanywa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi cha Mtakatifu Fransisko (SFUCHAS)kurekebisha mapungufu ya ubora yaliyokuwa yamebainishwa.

Aidha Tume imeruhusu Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Sayansi cha Mtakatifu Fransisko (SFUCHAS) kuanza kudahili wanafunzi wapya kuanzia mwaka wa masomo 2020/2021 baada ya kurekebisha mapungufu yake ya ubora aliyokuwa yamebainishwa huku Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU ) kimeendelea kuwa chini ya uangalizi maalum na Tume na kutoruhusiwa kudahili wanafunzi wapya.

Aidha kufikia Oktoba 2019 takribani vyuo vikuu vinane kati ya 19 vilivyokutwa na kasoro na kusitishwa kudahili wanafunzi wapya vimeruhusiwa kudahili na kuendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya programu  za masomo.

Akitaja vyuo hivyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika  Tanzania (UAUT),Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),Chuo Kikuu cha Askofu Mkuu Mihayo Tabora(AMUCTA),Chuo cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUK), na Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian(MARUCo).

Alisema vyuo vingine niChuo Kikuu Kishiriki cha Uhandisi na Teknolojia cha Mtakatifu Yosefu(SJUCET),Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi(SMMUCo).
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) Prof. Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Aprili 21,2020 wakati akitoa taarifa kuhusu maamuzi ya Tume hiyo kurejesha udahihili, kuendelea kusitisha udahili wa wanafunzi wapya na kufuta udahili  kwa baadhi ya Vyuo Vikuu nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa uratibu na udahili wa TCU,  Dk, Kokuberwa Mollel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...