Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa NHIF Bw. Hipoliti Lello akitoa mada kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha kuhusu mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya vilivyozinduliwa hivi karibuni.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Christopher Mapunda akiongea na waandishi wa habari kuhusu mpango wa Vifurushi vya Bima ya Afya ambapo aliwaeleza kuwa mpango huu utajumuisha kundi mkubwa la watanzania ambao wapo nje ya mfumo wa Bima ya Afya.
Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu akiongea na waandishi wa habari Mkoa wa Arusha ambapo aliwasihi kuwa mabalozi wazuri wa mpango huu wa vifurushi vya Bima ya Afya.
******************************
Mfuko wa Taifa wa bima ya leo umekutana na waandishi wa habari mkoani Arusha kwa lengo la kuwaelimisha kuhusiana na vifurushi vipya vya bima ya afya. Akiongea wakati wa Mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Christopher Mapunda amesema kuwa mpango huo una lengo la kuhakikisha idadi kubwa ya watanzania wanakuwa na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wa matibabu.

“Uanzishaji wa mango huu wa Vifurushi vya Bima ya afya ni fursa kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kuanzia kiwango cha 192,000 na kuwawezesha kupata huduma ya uhakika wa bima ya afya.

Aidha, Bw. Mapunda alisema kuwa NHIF imeendelea kutoa elimu kwa umma wa watanzania kuona umuhimu wa kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu ya uhakika.

Akiongea kwa niaba ya Waandishi waliohudhuria Mkutano huo Mwenyekit wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu alisema kuwa kwa jinsi hali ilivyo sasa ni muhimu kwa kila mwananchi kujiunga na mpango huu wenye nia ya kuwasaidia wananchi wengi zaidi.

“Hatukuwa tunaelewa namna vifurushi hivi vinavyofanya kazi, ila baada ya elimu hii nimeona ndio suluhisho, watanzania waone umuhimu wa kujiunga, kwasasa gharama za matibabu kwa sasa ni kubwa sana ila kwa vifurushi hivi kwa mfano 192,000 inakuwezesha kupata matibabu kwa mwaka mzima”-Alisema Bw. Gwandu.

Naye Meneja wa NHIF Mkoa wa Arusha Bw. Isaya Shekifu amewashukuru waandishi waliohuria kikao hicho na amewasihi kuwa mabalozi wazuri wa vifurushi vipya vya bima ya afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...