Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya usajili wake kukamilika na rasmi kutangazwa na Klabu ya Aston Villa, Mshambuliaji wa Kimataifa na Nahodha wa timu ya Taifa ya Tsnzania Mbwana Samatta amewashukuru watanzania kwa ujumla

Samatta amewaomba watanzania waendelee kumuombea ili afanye vizuri katika kibarua chake kipya ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Pia, Samatta amewashukuru mashabiki wa Genk kwa kuishi nao vizuri katika kipindi cha miaka minne alichokuwa anacheza kwenye klabu hiyo

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amempongeza nahodha huyo kwa hatua kubwa aliyoipiga na kuendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania vizuri.

Mwakyembe amesema, kwa sasa Samatta anaendelea kufungua njia kwa wachezaji wengine kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Akiongelea suala la kujengewa sanamu lenye picha ya Samatta, Mwakyembe amesema kwa sasa bado mshambuliaji huyo anatakiwa aendelee kujituma ili afike mbali zaidi jambo la Kujengewa sanamu ni la baadae.

Mbali na Samatta kuwashukuru mashabiki,watu maarufu na wachezaji mbalimbali wamempongeza Samatta kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Kitanzania kusajiliwa na timu ya Ligi Kuu  Uingereza.

Watu hao wamemtakia kila kheri kwenye kibarua chake kipya ndani ya Klabu ya Aston Villa ambapo leo kinashuka dimbani leo kucheza na Watford ingawa Samatta hataweza kucheza kutokana na jina lake kuchelewa kupelekwa bodi ya Ligi.

Mchezo wa Kwanza wa Samatta utakuwa ni dhidi ya Leicester City utakaochezwa wikiendi hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...