*Yaanzisha mpango ya uongezaji wa virutubishi vyakula,Mafuta na Madini Joto katika Chumvi

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

TAASISI ya Chakula la Lishe (TFNC), imepata mafanikio mbalimbali ya kuhakikisha jamii inapata lishe bora ili kuwa na nguvu kazi yenye tija kwa Taifa .Nguvu kazi hiyo ni pamoja na kuanzisha   mpango wa kuongeza virutubisho katika vyakula, kibaiolojia na kwenye mafuta na chakula pamoja chumvi kuongeza madini joto.

Mipango ya TFNC imefanikiwa ni  kwa kushirikiana na wadau wa kilimo  kuhamasisha ulimaji na utumiaji wa mazao yaliyoongezwa virutubishi kama viazi lishe na mahindi lishe  vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin A na Maharage yenye vitamini yenye madini chuma na zinki.

Mkurugenzi Mtendaji wa TFNC, Dk. Germana Leyna, aliyasema  hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya maoafisa mawasiliano wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuelezea mafanikio katika kampeni ya 'Tumeboresha Sekta ya Afya' kwa kipindi ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.


Lengo la kampeni hiyo ni kuangazia miaka minne ya Serikali na mafanikio yaliyopatikana katika sekta za afya nchini pamoja na uwekezaji wa miundombinu na Vifaa kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.

Dk. Leyna alisema lengo la kuanzisha mpango huo ni kupunguza udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kutoka asilimia 32 zilizopo sasa hadi kufika chini ya asilimia 20; kupunguza utapia mlo kutoka asilimia 3.5 za sasa hadi chini ya hapo na kupunguza tatizo la upungufu wa damu kwa wajawazito kutoka asilimia 29 hadi kumaliza tatizo.

"Kwa kushirikiana na sekta ya binafsi tumetekeleza kanuni za kuongeza virutubisho kwenye chakula. Kwa sasa tunaongeza virutubisho vya Vitamin A kwenye mafuta ya kula, Vitamin B 12, Zinki, Asidi ya foliki na madini chuma kwenye unga wa ngano na mahindi. Pia tunaongeza madini joto kwenye chumvi," alisema Dk. Leyna.

Amesema  wanashirikiana pia na wadau wakiwamo wazalishaji wadogo wa chumvi na viwanda vidogo vya kuzalisha bidhaa zinazoongezewa madini.Dkt Leyna  amesema mafanikio  waliyoyapata ni kufanikiwa  kuhamasisha ongezeko la bajeti ya lishe katika halmashauri kutenga Sh. 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe katika maeneo yao badala ya sh.500 iliyokuwa ikichangiwa katika afua hiyo.

Amesema awali halmashauri zilikuwa zikitenga Sh. 500 lakini kuanzia mwaka 2018 bajeti iliongezeka hadi kufikia Sh. 1,000 sawa na takribani Sh. bilioni 11 kwa nchi nzima.

Aidha, amesema wameboresha utoaji elimu ya lishe Kwa walengwa kupitia mkoba wa siku 1,000 unaojiendesha wenyewe kwa kuchangisha fedha za utengenezaji wa mikoba kwa ajili ya kupeleka elimu kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa mtoto kuanzia akiwa tumboni kwa mama yake, kuzaliwa mpaka kufikisha miaka miwili.

"Mkoba ni muhimu kwa sababu kipindi hiki ni muhimu mtoto kupata mahitaji yote ya lishe ikijumuisha virutubushi ili kuboresha ukuaji wake kimwili na kiakili,amesema Dk. Leyna.

Amesema tafiti walizofanya zinaonyesha kuwa mtoto akikosa lishe au virutubishi katika umri huo  anapata athari za kudumu za kimwili na kiakili ambazo haziwezi kurekebishika katika kipindu chote cha uhai wake.Alisema athari nyingine ni mtoto kuwa na uwezekano wa kupata magonjwa wasiyo ya kuambukiza pindi anapokuwa mtu mzima.

Dkt Leyna amesema  mkoba huo wenye maelezo yote unatumika kufundishia wajawazito na wawanake wenye watoto namna bora ya kuitunza mimba na mtoto mchanga na iana ya vyakula vya kumpa ili kumpa afya njema.

 Msanifu wa maabara kitengo Cha mikrobiolojia, kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dorah Chilumba akifanya upimaji wa kiwango Cha vitamini B9 (asidi ya foliki) kwenye sampuli za damu
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Dkt.Germana Leyna akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Maafisa Habari na Uhusiano wa wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kuhusiana na mafanikio ya Taasisi katika kipindi cha Miaka Minne katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Elimu na Mafunzo ya Lishe wa Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Sikitu Kihiga akizungumza mkoba wa siku 1000 Juu ya namna kutumia mama mjamzito.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Dkt. Germana Leyna akionesha mkoba wa siku 1000 kwa maafisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) walipotembelea taasisi hiyo tarehe 20 januari, 2020.
 Mkuu wa Idara ya Sera na  Mipango wa Taasisi ya Chakula na Lishe ( ATFNC) Adam Hancy  akizungumza kuhusiana na Mipango ya kufika jamii kuhusiana na Lishe.

Msanifu Maabara chumba cha mashine za maabara TFNC Job Kijungile akipima kiwango Cha madini mbalimbali kwenye sampuli za vyakula kwa kutumia mashine ya kisasa iitwayo microwave plasma atomic emission spectrometer (MP-AES) .
 Mashine ya mbalimbali zilizofungwa katika Taasisi ya MOI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...