Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi Mkuu wa
kitengo cha cardiovascular radiology ambaye pia ni Daktari bingwa wa
magonjwa ya moyo Engerasiya Kifai mashine ndogo ya kiganjani (V-Scan
dual) ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram), kupima
mishipa ya damu na ultrasound ambayo Taasisi hiyo imepewa msaada na
kampuni ya Computech30.Kulia ni Sandip Datta ambaye ni Meneja Mkuu wa
kampuni ya Computech30.
Mkuu wa kitengo cha cardiovascular
radiology ambaye pia ni Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Engerasiya Kifai akiangalia mashine ndogo
ya kiganjani (V-Scan dual) ya kuangalia jinsi moyo unavyofanya
kazi (Echo Cardiogram), kupima mishipa ya damu na ultrasound ambayo
Taasisi hiyo imepewa msaada na kampuni ya Computech30.Mashine hiyo yenye
thamani ya shilingi milioni 22 itatumika kwa wagonjwa walioko wodini na
wakati wataalamu wa Taasisi hiyo watakapokwenda kwa wananchi kutoa
huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo (Outreach program) .
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akipokea msaada wa mashine ndogo ya kiganjani (V-Scan dual) ya kuangalia
jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiogram), kupima mishipa ya damu
na ultrasound kutoka kwa Sandip Datta ambaye ni Meneja Mkuu wa kampuni
ya Computech30.Mashine hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 22
itatumika kwa wagonjwa walioko wodini na wakati wataalamu wa Taasisi
hiyo watakapokwenda kwa wananchi kutoa huduma za upimaji wa magonjwa ya
moyo (Outreach program) .
Picha na JKCI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...