Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Mhandisi Kadaya Balyhye akitoa maelezo kuhusiana utaratibu wa leseni kwa mafundi zinazotolewa na mamlaka hiyo. 
 Mkuu wa Kanda ya mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na mafundi simu mkoa Morogoro kuhusina na umuhimu wa mafundi simu kuwa leseni.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba akitoa maelezo kuhusiana na mafundi siku kuwa leseni katika mkutano. 


Baadhi ya mafundi Simu wa mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano uliohudhuriwa na Watendaji wa TCRA na Manispaa Morogoro. 

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa Mafundi simu wote wanatakiwa kuwa na leseni kutoka mamlaka hiyo ikiwa ni pamoja na kuwa na weledi wa kazi wanazozifanya. 

Akizungumza na mafundi simu wa Manispaa ya Morogoro Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania , Mkuu wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa mafundi simu ni kazi nyeti hivyo lazima wawe na leseni kazi hiyo na kuendelea kutengeneza simu bila leseni ni kosa la jinai. 

Amesema kuwa mafundi simu hao wanatakiwa kupata leseni ikiwa ni kupatiwa mafunzo kwa TCRA kushirikiana na wadau ambao na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi pamoja na Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam. 

Odiero amesema mafundi simu wakiwa na mafunzo watakuwa ni watu wa kulinda usalama wa mawasiliano ikiwemo kuweka utaratibu wa kuwa na vitabu vya kusajili simu na kuuliza historia ya simu  kabla ya kutengeneza kwa wateja wao simu walikozitoa ili kuondoa wizi wa simu. 

“Hakuna sababu ya fundi simu kutengeneza simu ambayo mwisho wa siku taarifa za simu hazieleweki ndipo hapo mtu anaingia katika tatizo lisilomhusu lililotokana na kushindwa kutokuwa na taarifa za simu ya mteja”amesema Mhandisi Odiero. 

Aidha amesema kuwa kwa mafundi simu kuwa na umoja kutarahisisha TCRA kufanya mawasiliano kwa mafunzo ambayo yatakuwa yameandaliwa ya kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kuzingatia matumizi ya simu kutoka kwa wateja. 

Nae Afisa Mwandamizi wa Huduma za Leseni Ipyana Haraba amesema kuwa mafundi simu ni watenda kazi hivyo ushirikiano unahitajika kutambua wanaofanya nje ya utaratibu na sheria itashika mkondo wake. 

Mhandisi Baluhye amesema kuwa mafundi simu nchini wakisajiliwa ni fursa ambapo serikali iko katika uchumi wa viwanda hivyo kunaweza kutokea kiwanda cha simu au kuunganisha simu mafundi wataotumika ni wa ndani. 

Mwenyekiti wa Mafundi Simu Mkoa wa Morogoro Ipyana Haraba amesema wameweka mkakati wa wa mafundi simu wote wawe wamejisajili katika umoja huu kurahisisha utoaji huduma na mafunzo ya weledi yatakyotolewa na TCRA. 

Haraba amesema kuwa safari imeanza kwa mafundi simu kuweka utaratibu wa mazingira ya kufanya kazi na vyombo vingine ikiwemo jeshi la polisi kushiriana katika kubaini wezi wa simu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...