Dr.Abballah Possi Balozi wa Tanzania nchini ujerumani akiwa na Mwalimu Bi.Venessa Fölsen Kiongozi Mkuu  wa Umoja wa Tanzania Ujerumani


 
 

Mwenyekiti wa Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani (UTU ) Mwalimu Bi.Venessa Upendo Fölsen siku ya jumamosi aliongoza kamati ya uongozi wa umoja huo katika kikao cha kukutana na balozi wa Tanzania nchini ujerumani Mhe. Dkt.Abdallah Possi katika ubalozi wa Tanzania mjini Berlin
 
Ubalozi uliwakaribisha kwa mikono miwili na kufanya mazungumzo nao ambayo Kiongozi wa umoja wa Tanzania Ujerumani amelezea kuwa Umoja huo utaitangaza Tanzania nchini ujerumani kwa nguvu zote kwa maslahi ya Tanzania na watanzania,ususani katika sekta ya Utalii,uwekezaji,afya na elimu ni mojawapo ya mambo yakatayopewa kipau mbele,Umoja wa Tanzania nchini Ujerumani ndio mwamvuli pekee unawakusanya watanzania waishio nchini ujerumani na moja ya niya yake ni kuleta mshikamano wenye kuleta maslahi kwa watanzania ujerumani na nyumbani Tanzania.
 
Pia kwa upande wake Mheshimiwa Balozi Dkt. Abdallah Possi amewataka watanzania kuungana pamoja kwa maslahi yao na ya Tanzania,pia kujivunia utanzania wao kwa kuitangaza vema Tanzania katika nyanza zote na vivutio vyake katika tufe la dunia ili kufanikisha Tanzania ya Viwanda itakayokuza uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...