Mbunge wa jimbo la Ilala, Musa Azan Zungu akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa nyumba za maafisa, na Askali Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam.

Na Avila Kingo, Globu ya Jamii
MBUNGE wa jimbo la Ilala, Musa Azan Zungu, amewaasa watakao kukaa katika nyumba za maafisa na Askari Magereza wawe waadilifu.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa nyumba za maafisa na Askari Magereza zilizopo Ukonga jijini Dar es Salaam leo, nymba hizo imezinduliwa na Rais w Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Dkt. Magufuli.

"Sio mmepata mshahara mnatoka Banana mnajiokotea vitu mnaleta ndani humu mtajikuta mambo hayaendi kwahiyo mkiingia humu ndani ingizeni wake zenu ili kuwe na heshima kwa aliyejenga, aliyetoa pesa, na heshima ya Mwenyezi Mungu na mashekhe na mapadri waliokuja hapa" amesema Zungu.

 Zungu amesema kuwa nymba hizo zimeombewa na mashekhe, Paroko na maaskofu kwa hiyo wawe waadilifu kwenye nyumba hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...