SHIRIKA
la umeme Tanzania TANESCO kupitia idara
ya masoko imeanza zoezi la kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya na vijiji vya mkoa
wa Tabora.
Lengo
la utoaji huo wa elimu ni kuwaelimisha wananchi wanaopitiwa na mradi wa REA
awamu ya tatu(REAIII) kufahamu taratibu za kuunganishiwa umeme pamoja
kuchangamkia fursa za mradi kabla hazijaisha. Miongoni mwa wilaya ambazo tayari
zimepitiwa na na sasa ziko kenye zoezi hilo la kupatiwa elimu ni wilaya ya
Uyui, Sikonge, na baadae zitafuatiwa na wilaya ya Nzega na Igunga.
Wananchi hao pia walipatiwa elimu kuhusu kifaa cha UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao hususan zile zinye ukubwa wa wastani w avyumba viwili na sebule.
Wakizungumza
wakati wa utoaji elimu kwenye vijiji vya Kagera, Ibiri, Msimba, Msuva, Mtakuja,
Songambele na Kasandalala baadhi ya wananchi wamesifu jitihada za serikali za
kuwaunganishia umeme kwa gharama ya shilling 27,000/= na tayari badhi yao
wameshanufaika na mrafi huo wa umeme.
Afisa Uhusoiano na Huduma kwa wateja Tanesco mkoani Tabora Bw. Lucas Swere akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya umeme wakati wa kampeni ya kuhamasisha wanavijiji kuunganisha umeme mkoani Tabora.
Aafisa masoko kutoka TANESCO Neema Chalila Mbuja akitoa elimu ya matumizi bora ya umeme na usalama wa umeme Kijiji cha Kagera na Songambele.
Aisa Masoko wa Tanesco, Bi. Neema Chalila Mbuja, (kushoto), akiungana na watoto wa kijiji cha Kagera na Songambele wakifurahia zawadi ya madaftari waliyopewa baada ya kujibu maswali yaliyoulizwa na wataalamu wa TANESCO baada ya kupatiwa elimu hiyo.
Wanakijiji wakifuatilia kwa makini elimu iliyokuwa ikitoelwa kwao kuhusu masuala ya umeme.
![]() |
Afisa masoko, Tanesco Bi. Jenifer Mgendi Maziku akitoa elimu ya namna ya
kutumia kifaa kiitwacho UMETA yaani umeme tayari anbacho kinafaa kutumiwa na
wananchi bila kufanya wiring kwenye nyumba zao
![]() |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...