Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimkaribisha Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akimuelezea jambo katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi na Programu za Ushirikiano wa Kikanda Kutoka Ofisi za Jumuiya ya Maziwa Makuu Burundi, Bw. Parek Madout kwa pamoja wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika, Bw. Aniefiok Johnson akimueleza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Uchumi na Programu za Ushirikiano wa Kikanda Kutoka Ofisi za Jumuiya ya Maziwa Makuu Burundi, Bw. Parek Madout

***************************
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Watumishi wa Ofisi za Mwakilishi wa Kudumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maziwa Makuu Barani Afrika Bw. Aniefiok Johnson katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Bw. Johnson pia ametumia nafasi hiyo kuhamasisha wadau wa uwekezaji nchini kushiriki Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji la Jumuiya linaloratibiwa na Jumuiya ya Maziwa Makuu. Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 18-23 Machi mjini Kigali, Rwanda na kuhudhuriwa na washiriki takribani 1000 Kutoka nchi mbalimbali duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...