NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa ametoa rai kwa mamlaka na taasisi zinazohusika na Viwanda likiwemo Shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO, DIT NA NEMC kuwa karibu na wawekezaji kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu na mazingira.

Aliyasema hayo ,wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Mji Kibaha ,mkoani Pwani, ambapo pia ameridhishwa kwa namna mji huo unavyotekeleza sera ya uwekezaji wa viwanda kwa vitendo .
 Bashungwa alieleza ,wawekezaji wa ndani na wa nje wanahitaji huduma muhimu bila kuwepo urasimu ili kuinua sekta ya uwekezaji.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya mji huo,Jenifa Omolo, aliyewakilishwa na Rosemary Msasi ,alisema halmashauri hiyo imetenga eneo maalum la viwanda vikubwa lenye ukubwa wa ekari 1,246 eneo la Zegereni umbali wa kilomita 4.5 kutoka barabara kuu iendayo Morogoro kutokea Dar-es-Salaam.
 Jonas Nyagawa, Mkurugenzi wa kampuni ya BM Motors inayounganisha mabasi Makubwa yenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 50 amemsifu Omolo kwa wepesi wa kuwamilikisha maeneo ya uwekezaji mara tu wanapokamilisha taratibu za kiserikali na kwamba hiyo inawamotisha wawekezaji wote.

”Mimi eneo langu lina ukubwa wa zaidi ya mita za ujazo 1800, lakini tayari nina hati milki na sibughudhiwi na mwingine kwenye eneo langu” alisema Nyagawa.
Bashungwa alieleza ,kiwanda hicho ni kikubwa na chenye tija kwa taifa huku akibainisha faida zitakazopatikana kuwa ni pamoja na kuilipa kodi serikali, kutoa ajira kwa watanzania na kuvinufaisha viwanda vingine kwani asilimia 45 ya malighafi zinazotumika kwenye kiwanda hicho zinapatikana nchini.

Awali, Bashungwa aliitembelea kampuni nyingine ya wawekezaji wa kitanzania ya GF VEHICLE ASSEMBLIES eneo la TAMCO inayotarajiwa kuweka kiwanda cha kuunganisha magari mchanganyiko yenye uzito usiozidi tani 8 na kwamba uzinduzi wake utafanyika mwezi Mei, 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo ,Imran Karmali alimweleza Waziri Bashungwa kuwa kiwanda hicho zaidi ya kutoa kodi kwa serikali pia kitatoa ajira.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...