
Msimu wa 17 wa Sauti za Busara umeanza rasmi leo Alhamis ya Februari 13 hadi 17 utakaofanyika eneo la kihistoria Ngome Kongwe likiwa na wadhamini mbalimbali ikiwemo Benki ya CRDB. Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Marumaru, Stone Town, Zanzibar mwakilishi wa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Zanzibar Ndugu Jerome Saraka ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Makusanyo ya VISA uwanja wa ndege amesema: "Leo tunapotambulisha rasmi udhamini huu wa milioni 20, tunadhamiria kulenga mambo makubwa matatu, moja kuongeza nguvu katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi yetu katika tamasha hili la Sauti za Busara, mbili kushiriki katika juhudi za kufungua milango ya uwezeshaji kiuchumi kupitia watalii ambao watakuwa wakihudhuria katika tamasha hili la Sauti za Busara na tatu kushiriki katika juhudi za kutambulisha vipaji vya muziki na uigizaji ambavyo ni sehemu kubwa ya ajira kwa vijana wa taifa hili.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...