Mwendesha Boda boda Nissa Mkimwa akiwa amempakia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu - Jenista Mhagama wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB Masta Boda iliyofanyika kwa Mkoa wa Ruvuma Peramiho wilayani Songea juzi. Waliosimama kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea – Pololet Mgema, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini – Janeth Shango, Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Benedicto Baragomwa na Meneja wa NMB Songea – Daniel Zake.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu - Jenista Mhagama akilipa nauli ya Boda Boda kwa kutumia QR Code kwa mwendesha Boda Boda wa Songea –Nissa Mkimwa Kwenye uzinduzi wa Masta Boda mjini Peramiho, wilayani Songea. NMB wamezindua kampeni ya MastaBoda mjini Peramiho ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yao iliyozinduliwa mwaka jana jijini Dar es Salaam na hivyo kuamua kuzindua kampeni hiyo nchi nzima.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu - Jenista Mhagama pamoja na viongozi wa Benki ya NMB wakicheza kwa Furaha wimbo maalumu wa NMB ulioimbwa kwenye Uzinduzi rasmi wa muendelezo wa kampeni ya NMB Masta Boda boda iliyofanyika Peramiho mjini Songea juzi.


=========   =============

Vijana nchini wametakiwa kuchangamkia fursa za NMB Mastaboda zinazoambatana na mikopo, zawadi za fedha taslimu na boda boda ili kukuza na kurasmisha biashara zao.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu - Jenista Mhagama kwenye uzinduzi wa NMB Mastaboda uliofanyika Peramiho nje kidogo ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma juzi na kukutanisha wendesha boda boda zaidi ya 200.

Amesema sekta ya boda boda kwa sasa inaheshimika na kutambulika kama ajira rasmi na hivyo wahusika hawana budi kutumia fursa hiyo kujinufaisha.

Kupitia kampeni ya Mastaboda, waendesha bodaboda wamerasmishwa na hivyo kuweza kuaminika na kupewa msaada kupitia mikopo ya fedha hata ya vyombo vya kazi kama pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu. Amesema kuwa kwa sasa Serikali inatambua sekta hiyo kuwa rasmi na kuahidi vijana wote nchini kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kushirikiana na wabia kama Benki ya NMB.

Akiongea kwenye uzinduzi huo, Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Benedicto Baragomwa aliwahakikishia wendesha bodaboda na serikali kuwa huduma hiyo itatoa fursa kwa maelfu ya waendesha boda boda nchini kwa kutumia huduma za Benki hatua itakayoimarisha usalama wa fedha na mali zoa.

“Kwa mkoa wa Ruvuma pekee, tumepanga kuwafikia wendesha boda boda Zaidi ya elfu 85 ambao mbala na malipo kupitia QR Code, pia wataweza kupata fursa ya mikopo na kuendeleza biashara zao Zaidi.” Alisema Baragomwa.

Aliongeza kuwa mfumo huu utawasaidia pia madereva boda boda kukuza biashara zao kwa kuwapunguzia adha ya kuhifadhi fedha taslim na kuwapa fursa ya kuepuka matumizi yasiyokuwa na mpangilio.

“kwa kutumia Mastercard QR, tunatoa huduma ya uhakika ya malipo kwa madereva boda boda kutoka kwa watoa huduma wote wa Benki za biashara wanaotumia huduma hii. Malipo yatafanywa kwa simu ya mkononi yenye program ya MasterCard QR na kupunguza hatari za kumiliki fedha taslim.” Alisema Baragomwa.

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Pololet Mgema ameipongeza NMB kwa kuanzisha huduma hiyo ambapo amewaomba waendesha bodaboda kujiunga na huduma hiyo sanjari na kuchukua vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo vitawawezesha kupata mikopo kupitia NMB.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...