Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipata maelezo
kuhusu biashara ya ngozi kutoka kwa mfanyabiashara na mfugaji Bw. Jonath
Magige wakati wa maonesho ya wafanyabiashara walioshiriki katika
mkutano wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza
changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Wilaya ya
Musoma Mjini Mkoa wa Mara.

Naibu Waziri
Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akijibu hoja za
wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara wakati wa Kongamano lao la
kueleza changamoto na kupatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Mkuu wa
Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima wakiangalia viatu vya ngozi
vinavyotengenezwa na wafanyabiashara wa mkoa huo, wakati wa maonesho ya
wafanyabiashara wakati wa Mkutano huo.

Mkuu wa Mkoa wa
Mara Mhe. Adam Malima akitoa maelezo kuhusu mkoa wake wakati wa Mkutano
wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza
changamoto za wawekezaji na wafanyabiashara na kuzipatia ufumbuzi
uliofanyika katika Mkoa wa Mara Februari 24, 2020.

Mfanyabiashara
mkoa wa Mara Bw. Edward Masato akichangia hoja wakati mkutano wa
mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto
za wawekezaji na wafanyabiashara uliofanyika Februari 24, 2020.

Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angelah Kairuki akioneshwa nyavu
inayotumika kuvulia samaki na Mvuvi Bw. Msendo Mwigine wakati wa mkutano
wa wa mashauriano kati ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza
changamoto za wawekezaji katika Mkoa wa Mara.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa mkuano huo.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
****************************
MWANDISHI WETU MUSOMA
Wafanyabiashara
na wawekezaji wa Mkoa wa Mara wameelezea kero mbalimbali zinazochangia
kukwamisha ukuaji wa uwekezaji mkoani humo ikiwemo tatizo la umeme na
wengine kueleza changamoto za utitiri wa kodi.
Wameeleza
changamoto hizo Februari 24, 2020 wakati wa mkutano wa mashauriano kati
ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikiliza changamoto za wawekezaji na
wafanyabiashara wa mkoa wa Mara uliohusisha Mawaziri na Manaibu Mawaziri
kutoka Sekta mbalimbali ikiwemo Viwanda na Biashara na masuala ya
Fedha wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu
anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki
uliofanyika Wilaya Musoma Mjini katika Mkoa wa Mara.
Lengo la
mkutano huo lilikuwa kusikiliza changamoto na kero wanazokabiliana nazo
katika maeneo yao ya biashara na uwekezaji na kuzitatua, ambapo
wameeleza namna utitiri wa kodi na kukatikatika kwa umeme kunavyochangia
uzorotaji kwa ukuaji wa uchumi na kuiomba Serikali kushughulikia tatizo
hilo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Wafanyabiashara
hao walieleza kuwa, kukosekana kwa umeme wa uhakika umekwamisha
shughuli za uzalishaji ikiwemo zile za viwandani.
Kufuatia hali hiyo wameiomba Serikali kutatua kero hiyo huku wengine wakibainisha hasara wanazopata katika changamoto hiyo.
Akieleza
changamoto za uwekezaji Dkt. John Changwa alieleza kuwa, TANESCO
imechangia kukwamisha uzalishaji katika viwanda kutokana na umeme
kukatika mara kwa mara pamoja na kutofika kwa wakati katika viwanda
vidogo kwa kuhusisha changamoto ya miundombinu hafifu ikiwemo barabara.
“Ni kweli
kabisa TANESCO hamtutendei haki kwani mmekuwa mnatukwamisha kwa muda
mrefu na mmeshindwa kufika kwa wakati hasa katika maeneo vinavyojengwa
viwanda huku vikiwa vihitaji huduma za umeme hivyo ni vyema mkabadili
utaratibu na kuona namna ya kutufikia kwa wakati,”Alieleza Dkt. Changwa
Akijibu
baadhi ya kero hizo kwa kushirikiana na mawaziri wengine Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametumia fursa
hiyo kuzikumbusha Mamlaka zote za Serikali za Mitaa nchini kusimamia
kikamilifu utekelezaji wa maamuzi ya Serikali kwa kuhakikisha changamoto
zilizoainishwa ikiwemo utitiri wa kodi, uwepo wa riba kubwa zinazotozwa
na benki, ucheleweshwaji wa vibali vya ajira, ukosefu wa ajira kwa
vijana, na uvuvi wa kutumia vyavu zisizokidhi mahitaji halisi na bei
elekezi kuwa juu.
‘’Ni wakati
sahihi kuendelea kuwahudumia wananchi kwa kuhakikisha tunatatua na
kumaliza kero zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara ili kuendelea
kuwa na maendeleo katika nchi yetu na niwahakikishie Serikali
imeendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwa na tija
inayotakiwa,”alisema Waziri Kairuki.
Sambamba na
hilo alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara wa mkoa huo kuendelea
kushirikiana na Serikali katika ulipaji wa kodi mbalimbali kwa utaratibu
uliopo na kuhakikisha wanachangia katika ukuaji wa pato la taifa.
“Serikali ya
Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
inasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya
watanzania na taifa kwa ujumla hivyo lazima tuzingatie na kutimiza
wajibu wetu ili kuepuka kuingia katika makosa yasiyo ya lazima na
kupelekea uwekezaji wenu kuwa wa hasara”,alisisitiza Waziri Kairuki.
Kwa upande
wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima alimhakikishia Waziri
kuendelea kutatua kero na changamoto katika mkoa wake ili kuwahakikishia
mazingira rafiki ya uwekezaji wao huku akiahidi kuendelea kusimamia
sheria zote zinazowahusu ili kuwa na tija katika kuwekeza mkoani humo
kwa kuzingatia fursa zilizopo.
“Mkutano huu
umekuwa wa faida sana kwa kuzingatia umetoa fursa kubwa kwa kuwakusanya
wafanyabiashara na wawekezaji 400 kwa pamoja na kuweza kuzieleza kero
zao, tunaahidi kero ambazo hazijapatiwa majibu kwa siku ya leo
zitatatuliwa haraka iwezekanavyo,”Alisisitiza Mhe. Malima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...