Na Amiri Kilagalila, Njombe
Wananchi wa kijiji cha Magoda halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe wameonyesha kutoridhishwa na uamuzi uliotolewa na mkuu wa wilaya Ruth Msafiri wa kuliachia kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya kusini, ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekari 580 kwa madai ya kwamba hawana sifa kisheria za umiliki wa eneo hilo.

Kufuatia agizo hilo ambalo limetolewa mbele ya mkutano wa hadhara, wananchi wanasema wanafikiri kwenda kuitafuta haki yao katika vyombo vya sheria kwani wao ndiyo wamiliki halali wa eneo hilo ambalo walitoa kwa shirika la NJODECO 1977 kwa ajili ya shughuli za kiuchumi ambapo baada ya kushindwa kuliendesha lilirejesha halmashauri ambayo ikaamua kumilikisha kwa kanisa .

Musa Muhagama na Gideon Mwautenzi mwenyekiti mstaafu wa kijiji wanasema eneo hilo limeporwa kwa wananchi kwani mchakato wa kulimilikisha kanisa ulifanyika kimakosa kwa kuwa wanapohitaji nyaraka za mauziano hazitolewi hivyo wanamuomba Rais kuingilia kati.

"Tunachokitaka ni namna gani kanisa wameingia pale,ili wananchi tupewe fidia zetu zinazotakiwa,sisi wananchi hatujaridhika na maelezo ya mkuu wa wilaya kwasababu ameongeza tatizo,tunachomuomba Rais atusikilize na mkuu wa wilaya sio mwisho wa sheria sisi tutaenda mbele"walisema wananchi

Awali katibu mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Grayson Shilongoji akifafanua kuhusu uhalali wa umiliki wao anasema kanisa lilipewa kisheria ardhi hiyo na halmashauri ya mji lakini pindi wanapotaka kuliendeleza wamekuwa wakikumbana na vikwazo kutoka kwa wananchi huku afisa ardhi halmashauri Lusumbilo Mwakafute akidai mmiliki ni kanisa .

"Halmashauri kwa kushirikiana na wizara ya ardhi ilimikisha eneo hili kisheria kwa dayosisi,kwa hati namba 12942"alisema Grayson Shilongoji

Baada ya kurejea kwenye sheria na vipindi vyote vya maboresho ya sheria ya ardhi tangu 1977 hadi 1999 ndipo mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akatoa ruhusa kwa kanisa kuendelea zake katika eneo hilo huku pia akipiga marufuku wananchi kuendelea kufanya uvamizi katika eneo hilo.

"kama umechimba shimo la kupanda miti tafadhali kauoe haraka,na ninawapa mwezi mmoja tu usipouhamisha sio haki yako,baada ya tarehe 20 mwezi ujao usisogee hapa na ukisoge zitafuata hatua nyingine,na walio kuwa wanachoma humu mkaa ni jinai,ila mkurugenzi atakuja kukagua halafu atajiridhisha eneo unalo sema ni lako na hio ni yako na mkurugenzi lakini wamiliki halali ambao ni KKKT waendelee na shughuli zao"alisema Ruth Msafiri

Kanisa la KKKT lilipewa na halmashauri zaidi ya ekari 1227 ambalo liliachwa na NJODECU `ambapo katika eneo hilo ekari 580 zinadaiwa kuwa zimepokwa kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...