DC Waryuba akisistiza Jambo kwa wananchi.
Wananchi wa Kijiji Cha Mivanga wakimsikiliza DC Waryuba
DC Waryuba (katikati) akiwa na wakuu wa Idara katika ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika Wilaya yake
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amewataka wakulima waliokopa pembejeo kulipa madeni hayo ili waweze kukopeshwa Tena katika msimu mpya
Hayo ameyasema wakati akijibu swali la mkazi wa Mikuyuni kata ya Nambahu Mkalavachi Mkalavachi kwenye muendelezo wa ziara ya Dc ya kusikiliza kero za wananchi na kukagua shughuli za maendeleo
Mkulima huyo aliomba pembejeo ziwafikie kwa wakati ili waweze kupulizia kwa muda muafaka kwakuwa zinapochelewa na uzalishaji unakuwa mdogo
"Wakulima waliokopa pembejeo msimu uliopita wengi hamjalipa madeni hayo hivyo taasisi walizowakopesha wanamsubiri mlipe ili wakopeshe tena dawa ya Deni ni kulipa ," alisema Waryuba
Alisema msimu unakaribia hivyo pembejeo zikiwahi ndivyo uzalishaji unavyoongezeka wa zao la korosho
Mbali na Hilo amewataka wananchi kulima na mazao mengine badala ya kutegemea zao moja la korosho kwakuwa ardhi inakubali na mazao mengine
" Huu ni msimu wa mvua sitarajii kuwaona akina baba na vijana vijiweni kwenye kahawa Wala mabonanza,nendenimkawasaidie akina mama shughuli za shamba," alisema Waryuba .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...