Kamishna wa Uhifahi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dkt. Freddy Manongi na baadhi ya wajumbe wa Menejimeti ya Mamlaka hiyo wamefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Ujirani mwema inayojengwa kwa Ufadhili wa Mamlaka hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa kituo cha Afya cha Arash kilichopo Loliondo ambapo NCAA imetoa mchango wa Shilingi Milioni 100 kusaidia ujenzi huo.
Dkt Manongi aliyeongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Rashid Taka pia walitembelea maendeleo ya ujenzi kambi ya Jeshi ya Kiteule iliyoko Loliondo Mkoani Arusha ambapo NCAA imechangia kiasi shilingi milioni 200 ikiwa na kuunga mkono juhudi za Jeshi la Wananchi kuimarisha ulinzi na Usalama hasa maeneo ya mipakani.
Katika ziara hiyo Dkt Manongi na Ujumbe wake pia walipata fursa ya kutembelea hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro ili kuona maendeleo ya ujenzi ulipofikia na kuahidi kuwa NCAA itaongezea shilingi milioni 30 ili kukamilisha kazi ya ujenzi wa vyoo utakaowezesha hospitali hiyo kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Rashid Taka pamoja na Menejimenti ya NCAA wameridhishwa ujenzi wa hospitali ya Samunge ambayo NCAA ilichangia Shilingi milioni 400 katika ujenzi wake ambapo NCAA imeahidi kuendelea kutoa fedha zingine kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ili kusaidia uboreshaji wa huduma za jamii ndani na nje ya Hifadhi kama sehemu ya mchango kwa Jamii.
Aidha Mhe. Taka ameishukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa juhudi zake za kuendelea kusaidia miradi mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
Michango iliyotolewa na NCAA katika miradi hiyo ni sehemu ya miradi mbalimbali inayotolewa na Mamlaka hiyo katika kuwawezesha wananchi wanaoishi jirani na hifadhi hiyo kutambua mchango wao katika shughuli za Uhifadhi.
Kituo cha Afya Arash Kilichopo Loliondo Mkoani Arusha ambacho Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 100 katika Ujenzi wake

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...