Hatimaye Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu huko Sudan Kusini imeundwa baada ya Riek Machar kuapishwa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais wa nchi hiyo.

Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar na hasimu mkuu wa Rais Salva Kiir jana aliapishwa kuwa makamu wa kwanza wa rais, ikiwa ni uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

Uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Sudan Kusini umepongezwa kieneo na kimataifa na kutajwa kama hatua moja mbele ya kumaliza mzozo na vita vya ndani katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.

Hafla ya uundwaji wa serikali hiyo ilifanyika jana katika mji mkuu Juba ambapo Rais Salva Kiir na Riel Machar walisalimiana kwa tabasamu huku wakishangiliwa na wageni mashuhuri waliohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Machar na viongozi wengine kutoka vyama vya upinzani.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...