Aliyekuwa Afisa habari wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amewaomba mashabiki wa Klabu ya Yanga kujitokeza  kwa wingi kwenye mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup dhidi ya Gwambina FC inayoshiriki ligi Daraja la kwanza (FDL) uwanja wa Taifa Dar..

Muro ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, yuko likizo na ameamua kuitumia likizo yake kuungana na viongozi kurejesha amsha-amsha

Aesema kuanzia sasa mashabiki wa Yanga watembee kwa amani kwa sababu amerejea na password ya ushindi.

Amesema Iwapo Mashabiki wa Simba wakiwauliza kwa nini wanatoa sare nyingi ni kwa sababu wanaenda kuoa March 08.


"Nawaambia mashabiki kesho njooni kwa wingi uwanjani kuna suprise yenu, tunafungua ukurasa mpya kwa klabu yetu Ile kampa kampa tena tunaitaka kesho, tunataka ushindi wa kuanzia goli nane" amesema.

"Tumezungumza na kocha, wachezaji na tumewaambia kesho afe beki afe kipa, tunataka ushindi, viongozi wametimiza wajibu wao, wachezaji watimize wajibu wao na sisi mashabiki tutatimiza wajibu wetu,"amesema Muro.

 Amesema kuanzia leo, Yanga hawatalia tena, hawatakubali kuonewa wala kuhujumiwa na mtu yeyote na kuanzia leo watalinda uwanja kuelekea mechi ya Simba Machi 8 mwaka huu.

Aidha, Muro amewataka wadau wote waliokuwa viongozi wa timu hiyo kipindi cha nyuma, wajitokeze kuunganisha nguvu "Wale wote tuliokuwa sote wakati ule njooni tuunganishe nguvu. Viongozi wamefungua milango, tusibaki kulalamika tu kuwa timu inapotea. Wale mliokuwa mnamwaga upupu njooni mmwage, mliokuwa mkitoa magari, fedha njooni tufanye kazi tuirejeshe heshima ya klabu yetu"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...