Mali zilizokamatwa.

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali zao.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa usalama ali inayopelekea kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na ajali za barabarani. 

KUPATIKANA NA MALI ZIDHANIWAZO KUWA ZA WIZI. 
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia kijana DAVID MUSA [20] Mkazi wa Iyunga  Jijini Mbeya kwa tuhuma ya kupatikana na mali zidhaniwazo kuwa za wizi.
Tukio hilo limetokea tarehe 18.02.2020 majira ya saa 16:10 jioni huko Mtaa wa Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika msako uliofanywa na Jeshi la Polisi mkoani hapa na kumkuta mtuhumiwa akiwa na Kamera moja [01] aina ya Cannon 7D, Lens mbili [02] ndogo aina ya Canon 7D, simu ndogo nne [04] aina ya Tecno mbili, Itel moja na Samsung moja na laini tatu [03] za Tigo, Vodacom na Halotel mali zidhaniwazo kuwa za wizi. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI TOKA NDANI YA GARI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa watano 1. JOSEPH MOHAMED [38] Mkazi wa Airport ya Zamani, 2. PASCHAL JOHN [57] Dereva Hiace na Mkazi wa Mwambene, 3. MAWAZO SAMWEL [28] Dereva na Mkazi wa Mafiati, 4. IBRAHIM MAKOKULA [25] Mkazi wa Ilomba na 5. ZAWADI RICHARD [25] Mkazi wa Makunguru kwa tuhuma za wizi toka ndani ya gari.

Tukio hili limetokea tarehe 15.02.2020 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Stendi ya Mabasi Nanenane Jijini Mbeya baada ya Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kupata taarifa za kuwepo kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi toka ndani ya magari hasa kwa abiria ndipo ulifanyika msako kwa kushirikiana na viongozi wa Stendi ya Mabasi Nanenane na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na matukio hayo.
Aidha katika msako huo, yamekamatwa magari mawili yenye namba za usajili T.632 BQQ aina ya Toyota Hiace na T.780 CZT aina ya Toyota Hiace ambayo hufanya safari kati ya Stendi Kuu – Uyole ambayo yanatuhumiwa kwamba vitendo vya wezi kwa abiria hutokea.
Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa watuhumiwa wengine pamoja na gari moja ambalo limetajwa kuhusika katika matukio hayo.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI.
Jeshi la polisi mkoani mbeya linawashikiliae watuhumiwa wanne [04] 1. MASIKITIKO PATSON @ MBUZI [34] Mkazi wa Mtakuja 2. HURUMA MWASILE [36] 3. AMANI MSWIMA [21] Mkazi wa Mlima reli na 4. EZEKIA SINKALA [26] Mkazi wa Mtakuja kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio ya unyang’anyi, uporaji wa Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya.
Watuhumiwa wamekamatwa mnamo tarehe 12/02/2020 baada ya Jeshi la Polisi Mkoani hapa kufanyika msako maalum maeneo mbalimbali ya Mbalizi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao. Watuhumiwa wote wamehojiwa na kukiri kutenda matukio mbalimbali kama ifuatavyo:-
  1. Mnamo tarehe 20/12/2019 majira ya usiku huko Mtakuja mtu aitwaye ZACHARIA JACKSON [30] dereva bodaboda aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina ya T- BETTER yenye namba za usajili MC 149 CFJ.

  1. Mnamo tarehe 10/02/2020 huko MtakujaUtengule Usongwe mtu aitwaye   SHUKURU JUMA [26] aliuawa kisha kunyang’anywa pikipiki yake aina King lion.

  1. Mnamo tarehe 29/01/2020 huko ZZK Mbalizi majira ya usiku mtu aitwaye SADOCK NIMROD [21] dereva bodaboda alivamiwa na kisha kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kisha kunyang’anywa Pikipiki.

Upelelezi wa mashauri haya unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA WAHALIFU SUGU WA MATUKIO YA UVUNJAJI.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu wawili 1 .MAJALIWA  CHARLES [18] Mkazi wa DDC Mbalizi na 2. ANDWELE  ANDIGENIE MWAKAOISON [26] Mkazi wa DDC.
Tukio hili limetokea mnamo tarehe 19/02/2020 majira ya saa 17:00 alfajiri katika msako maalumu uliofanyika huko maeneo ya DDC Mbalizi, Kata na Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa na baada ya kuwapekua wamekutwa na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
  1. Televisheni mbili  inchi 52 aina ya hitech na inchi 32 aina ya samsung
  2. CPU mbili aina ya dell 
  3. Monitor mbili [2] aina ya samsung na dell 
  4.  Laptop moja aina ya hp 
Watuhumiwa wamekiri kuhusika kwenye matukio ya kuvunja nyumba usiku na kuiba. baadhi ya mali zimetambuliwa na wahusika.

            Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...