Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko akifafanua umuhimu wa ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara ya maafa, wakati akifungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambapo yeye ni mwenyekiti wa kikao hicho, leo tarehe 18 Februari 2020, Zanzibar.
 Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo akifafanua umuhimu wa Nchi  za SADC kuwa na mikakati ya kukabili maafa yanayo zikabili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar.
 Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi akifafanua namna ya nchi za SADC zinavyoathirika na maafa ya asili, wakati wa kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18 Februari, Zanzibar.
 Baadhi ya makatibu wakuu kutoka Tanzania, wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC, leo tarehe 18, Februari, 2020, Zanzibar, (katikati), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, anayeshughulikia Mifugo, Profesa,  Olesante Ole Gabriel (kulia kwake), Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dkt. Faraj Mnyepe,  na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.
 Baadhi ya maafisa waandamizi kutoka ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa, leo tarehe 18 Februari, 2020, Zanzibar.
Makatibu Wakuu na maafisa waandamizi wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, Februari, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”
 Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika ukanda wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC,wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, leo tarehe 18, 2020, ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”


“Tatizo la athari za maafa yanayotokana na majanga ya asili linahitaji ushiriki wa sekta zote ili kukabiliana nalo ipasavyo, katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)” Mwaluko.

Kauli hiyo imetolewa leo mjini Zanzibar na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji), Dorothy Mwaluko wakati alipokuwa anafungua kikao cha SADC cha Makatibu Wakuu wenye dhamana ya maafa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye yeye ni mwenyekiti.

 Mwaluko amesema nchi zote za SADC zina uzoefu wa masuala ya maafa, hivyo ni matarajio yake kuwa kazi waliyopewa ya kuandaa nyaraka kwa ajili ya mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya maafa utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 21 Februari 2020,  uweze kufikia malengo yake.

Katika kikao hicho, Makatibu Wakuu wataandaa nyaraka itakayo ainisha mikakati na programu za kukabiliana na maafa na mpango unaobainisha namna nchi za SADC zilivyojipanga kukabiliana na maafa yanapotokea katika ukanda huo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mtendaji wa SADC wa Masuala ya Ushirikiano wa Kikanda, Dkt. Thembinkosi Mhlongo  alieleza kuwa athari za maafa zikiwemo vifo, uharibifu wa mali na miundombinu zimezikumba takribani nchi zote za SADC. Hivyo amesisitiza umuhimu wa nchi hizo kushirikiana kwa pamoja kuandaa mikakati ya menejimenti ya maafa.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Bw. Abdallah Hassan Mitawi amewaeleza  wajumbe wa kikao hicho kuwa nchi za SADC zimelipa umuhimu mkubwa suala la kukabiliana na athari za maafa na hilo linadhihirishwa na ushiriki wa nchi 15 kati ya 16 wanachama wa SADC katika mkutano huo.

Mkutano huo unaofanyika kwenye Hoteli ya Madinat AL Bahir iliyopo Mbweni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar unatarajiwa kuhitimishwa kwa kikao cha ngazi ya Mawaziri tarehe 21 Februari 2020 ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kaulimbiu ya Mkutano huo : “Ushiriki wa kisekta kwenye Kupunguza madhara  ya maafa ni njia  bora ya kujenga Uhimili  katika ukanda wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...