Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakizungumza na mfungwa ambaye amepatiwa ujuzi gerezani wa fani ya ushonaji katika Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.
 Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitoka  katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kuendelea na ziara yao ya mfunzo katika maeneo mbalimbali ya Jeshi la Magereza.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza, SSP. Amina Kavirondo akiwasilisha andiko linalohusu majukumu ya Jeshi hilo mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(hawapo pichani).
Mkufunzi Mwandamizi  wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali  Cherestino Msolla (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga, ACP. Nsajigwa Mwankenja walipofanya ziara ya mafunzo katika Jeshi la Magereza jana Februari 12, 2020.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakitembelea sehemu mbalimbali katika Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga kama inavyoonekana katika picha.

Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali nkuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza ikiwemo program za urekebishaji, jana Jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha Askari wa Kikosi Maalum cha Magereza kikionesha onesho la ukakamavu mbele ya Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa(NDC) walipotembelea Makao Makuu ya Kikosi hicho jana, jijini Dar es Salaam.
Maafisa Washiriki kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa cha Tanzania wakiburudika na matunda ya madafu katika ziara yao ya mafunzo katika Jeshi la Magereza.
Kamishna wa Magereza, Uwesu Ngarama(wa pili toka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Washiriki waliotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jana(waliosimama mstari wa nyuma) kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(wa pili toka kushoto walioketi) ni Mkufunzi Mwandamizi  wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Bregedia Jenerali Cherestino Msolla (kushoto) ni Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremiah Katungu(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...