Mahasimu wa kisiasa nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar wamesisitiza kuwa wataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kufikia Jumamosi ya kesho (Februari 22) kama ilivyopangwa.

Wawili hao walitangaza hayo jana Alkhamisi, baada ya kambi hasimu wanazoziongoza kuhitalifiana kuhusu idadi ya majimbo ya nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.

Waasi nchini Sudan Kusini walipinga pendekezo la Rais Salva Kiir ambalo lingeipelekea nchi hiyo kurejea katika idadi ya awali ya majimbo kumi na nyongeza ya majimbo mapya matatu.

Itakumbukwa kuwa, kupunguza idadi ya majimbo nchini, lilikuwa moja ya matakwa makuu ya upinzani unaoongozwa na Riek Machar kwa ajili ya kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Baada ya kukutana na Kiir katika Ikulu ya Rais jijini Juba jana Alkhamisi, Machar alisema, "tumeafikiana kuunda serikali Februari 22."
 
Naye Rais Salva Kiir amesema atamteua Riek Machar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais leo Ijumaa, huku akiahidi kumdhaminia usalama mwanasiasa huyo pamoja na viongozi wengine wa kambi yake. Ameongeza kuwa, iwapo kuna masuala yenye utata na ambayo hawajakubaliana kufikia sasa, basi watayajadili ndani ya siku zijazo.

Mwaka jana, Rais Salva Kiir na Riek Machar walikubaliana kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kufikia Februari 22, baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu. 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...