Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

ZAIDI ya miili 6000 imepatikana katika makaburi ya halaiki nchini Burundi huku maiti 6032 na maelfu ya risasi yamegundulika katika makaburi sita ya halaiki katika eneo la Karusi nchini humo.

Mamlaka nchini Burundi imetangaza kugundua zaidi ya miili 6000 katika makaburi sita ya watu waliozikwa kijumuiya.

Yaliyogunduliwa katika eneo la Karusi ni makubwa kutokea tangu Serikali itangaze kuanza kwa kampeni ya kugundua makaburi hayo mwezi Januari 2014.

Pierre Claver Ndayicariye Mwenyekiti wa Kamisheni ya ukweli na maridhiano ya Burundi  amevieleza vyombo vya habari  kuwa mabaki 6032  pamoja na maelfu ya risasi yamegundulika na hiyo ni pamoja na nguo, miwani na rozari ambavyo vilitumika kuwagundua baadhi ya wahanga.


Ukirejea mauaji ya 1972 ambayo iliaminika kuwa iliwalenga watu wa kabila la Hutu, Ndayicariye amesema kuwa familia za wahanga  ziliweza kuvunja ukimya uliohifadhiwa kwa miaka 48.

Imeeleza kuwa Kamisheni hiyo iliundwa mwaka 2014 kufuatia jinai zilizofanyika mwaka 1885 hadi 2008 na hadi sasa wamegundua makaburi ya halaiki 4000 yenye miili 142,000 ya wahanga wa jinai ya vita.

Idadi hiyo kubwa ya makaburi kuwahi kutokea nchini humo iwewashtua watetezi wa haki za binadamu na kueleza kuwa jinai zizofanywa na Rais Pierre Nkurunzinza zifuatiliwe pia.

Si mara ya kwanza kwa makaburi ya jumuiya kugunduliwa nchini Burundi na Serikali ya Bujumbura pamoja na mashirika  yasiyokuwa ya kiserikali nchini Burundi yamekuwa yakipinga ripoti za mashirika ya kutetea haki za binadamu kama Amnesty International na Human Rights Watch yanayodai kuwa bado kunashuhudiwa  ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo.

 Machafuko yameendelea kuikumba Burundi tangu mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuteuliwa na chama chake cha CNDD-FDD kuwania tena urais kwa mara ya tatu  na baadaye chama hicho hivi karibuni kilimteua Katibu Mkuu wa chama hicho, Evariste Ndayishimiye kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotegemewa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...