Serikali ya Burundi imekiri kuua watu 22 ndani ya siku chache zilizopita, kwa tuhuma za kufanya 'makosa' yanayohusishwa na uchaguzi mkuu ujao.

Vyombo vya dola nchini humo vimeripoti kuwa, watu hao waliuawa katika mji mkuu Bujumbura, na kwamba maafisa wawili wa polisi wameuawa pia katika ghasia hizo za kabla ya uchaguzi.

Vyombo vya usalama nchini Burundi vimesema kuwa, vimewatia mbaroni watu sita wanaohusishwa na uhalifu huo wa kabla ya uchaguzi unaotazamiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo, Pierre Nkurikiye amethibitisha habari ya kutokea mauaji hayo katika wilaya za Nyabiraba na Isare viungani mwa Bujumbura na kuonya kuwa, "tutakabiliana na watenda jinai wanaotaka kutumia vibaya mazingira haya ya uchaguzi. Wananchi wawe watulivu kwani maafisa usalama wamedhibiti mambo."
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...