Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na
Uokoaji Chogo ,Kamishna Msaidizi,Kennedy Komba(kulia) wakati wa ukaguzi
wa mabweni yanayotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho kilichopo wilayani
Handeni mkoani Tanga,leo.Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin
Gondwe.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia),Mkuu wa Wilaya ya
Handeni,Godwin Gondwe (watatu kulia),Mbunge wa Handeni Vijijini,Mboni
Mhita(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo ,Kamishna
Msaidizi,Kennedy Komba(kulia), wakipita katika moja ya mabweni
yanayojengwa katika chuo wakati wa ziara ya naibu waziri leo kukagua
ujenzi wa mabweni wilayani Handeni mkoani Tanga.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin
Gondwe akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni(hayupo pichani),wakati wa kikao cha ndani kilichohusisha
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama baada ya naibu waziri kuwasili
wilayani Handeni leo kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na viongozi wa wilaya ya
Handeni,mkoani Tanga leo baada ya kuwasili katika kijiji cha Chogo kwa
ziara ya kikazi.Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Godwin Gondwe.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...