Na Luteni Selemani Semunyu

Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo ametangaza mashindano ya Tanapa Lugalo Open yanatarajiwa kufanyika Machi 14 na 15 Mwaka huu katika Viwanja vya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwandishi wa hbari hizi Mwenyekiti huyo alisema masindano hayo yalikuwa yafanyike February 29 na Machi Mosi lakini kutokana na baadhi ya Maandalizi kutokamilika imelazimu sasa kusogeza mbele.

“ Tumesogeza mbele ili kutoa fursa ya wachezaji wengi kutoka maeneo mbalimbali kuweza kufanya maandalizi na kushiriki hasa kwa wachezaji wanaotoka katika vilabu mbalimbali nje ya Jiji la Dar es salaam ambao walikuwa wakisubiria kwa hamu kubwa Mashindano hayo.” Alisema Brigedia Luwongo.

Aidha alisema pia Mgeni rasmi katika ufungaji wa Mashindano hayo anatarajiwa kutangazwa baadae katika mkutanona Waandishi wa habari mara baada ya kuthibitisha kuwepo katika mshindano hayo kulingana na ratiba zake.

Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kaptni Japhet Masai alisema tayari taaarifa zimeshatumwa kwa manahodha wa Vilabu mbali mbali na Dirisha limeshafunguliwa kwa yeyote anayetaka kushiriki kuweza kujiandikisha.

“ Mpaka sasa tunawachezaji zaidi ya 50 wameshajiandikisha ikiwa ni siku moja tangu kufunguliwa kwa zoezi la kujiandikisha hali inayoashiria mashindanohaya kuwa na mvuto zaidi mwaka huu ukilinganish na mwaka uliopita” alisema Kapteni Masai.

Kwa upande wa Wanawake nahodha wa Timu hiyo kwa Lugalo Hawa Wanyenche alitoa wito kwa Wanawake katika Vilabu mbalimbali na Nchi za Afrika Mashariki kujitokeza katika Mashindano hayo ya kwanza Makubwa katika Mwaka huu tangu vianze.

Tanapa Lugalo Open ni Miongoni mwa mashindano Makubwa yanayodhaminiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA na kuvutia wachezaji kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...