Yassir Simba, Michuzi Tv

MATUMAINIA ya timu ya soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam kuwamo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu yamezidi kuyeyuka baada ya mchezo wake wa leo dhidi ya Coastal Union a.k.a Wagosi Wakaya kumaliza kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo wa Yanga dhidi ya Coastal Union umefanyika leo Februari  23 mwaka huu wa 2020 ambapo kila timu ilionekana kuhitaji kuibuka na ushindi wa alama tatu lakini hadi dakika 90 zimalizika wamemaliza kwa kupata sare ambayo sasa unaifanya Yanga kufika alama 41 ikiwa imecheza michezo 22 hadi sasa.

Hata hivyo Yanga katika mchezo wa leo walionekana kucheza kabumbu safi na lenye ushindani mkubwa huku Coastal nayo wakionekana kupanga mashambulizi.Ufundi wa wachezaji wa timu zote mbili kulisababisha mchezo kuwa na ushindani mkubwa.

Kwa kukumbusha tu Yanga imeendelea kupata matokeo ya sare kwani huu ni mchezo wa nne mfululizo.Matokeo hayo ya sare wanaifanya Yanga kupoteza matumaini ya kutoa ubingwa kwani sasa iko nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi hiyo huku timu ya soka ya Simba wakiwa wanaongoza ligi kwa alama 62 na hivyo kuihakikishia kutetea ubingwa kwa msimu huu.

Hata hivyo Yanga bado wako nyuma kwa Michezo ambayo imecheza ikilinganishwa na Simba Simba ambayo imecheza Michezo mingi zaidi.

Wakati huo huo leo kuna Michezo mingine imechezwa katika Ligi hiyo ambapo maafande wa Tanzania Prisons imewaadhibu timu ya soka ya Lipuli FC magoli 2 kwa 0 .Magoli yamefungwa na wachezaji  Salumu Kimenya dakika ya 12 na Ismail Aziz dakika ya 90 huku Alliance wamechoshana nguvu na Singida United kwa sare ya 1 1 mabao Sameer Vicent dakika ya 10 na Stephen Kamwene dakika 53.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...