Mchunguzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyika, akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 
(Picha na Mtandao)

MCHUNGUZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyika (44) ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukumkutanisha na kamati inayoshughulika na suala na kukiri na kuomba msamaha kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mshtakiwa Batanyika ambaye anakabiliwa na makosa ya kushawishi rushwa ya zaidi ya Sh. milioni 300, kupokea na kutakatisha UDS 20,000 amedai hayo baada ya wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai mbele ya Hakimu  Mfawidhi, Godfrey Isaya kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Baada ya kueleza hayo, mshtakiwa Batanyika ameiomba mahakama hiyo kukutana na kamati ya inayoshughulika na kukiri na kuomba msamaha kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Akijibu hoja hizo wakili Simon alidai atafikisha kilio chake kwa kamati hiyo ili aweze kukutana nayo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Katika tarehe iliyopita, mshitakiwa huyo aliieleza mahakama kuwa  amemwandikia barua Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kwa ajili ya kukiri na kuomba msamaha kwa makosa yake.

Katika kesi hiyo inadaiwa Februari 9, mwaka huu huko Upanga, mshitakiwa akiwa mwajiriwa Takukuru kama Mchunguzi Mkuu, aliomba rushwa ya Sh milioni 200 kutoka kwa Hussein Gulamal Hasham kwa lengo la kuharibu ushahidi wa tuhuma za kukwepa kodi tuhuma zilizokuwa chini ya uchunguzi wa mwajiri wake.

Ilidaiwa  kuwa Februari 10, mwaka huu huko katika Viwanja vya Maonyesho ya Biashara, Sabasaba vilivyopo Temeke Jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alijipatia USD 20,000 kutoka kwa Faizal Hasham kama kishawishi cha kuharibu ushahidi wa tuhuma za kukwepa kodi dhidi ya Hussein Gulamal Hasham  zilizokuwa zinafanyiwa uchunguzi na Takukuru.

Pia Februari 13, mwaka huu katika ofisi za Makao Makuu ya  Takukuru, mshtakiwa akiwa mwajiriwa na Mchunguzi Mkuu wa Takukuru, alishawishi rushwa ya USD 50,000 kutoka kwa Thangavelu Nallavan Vall kama kishawishi cha kuharibu ushahidi wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili za kukwepa kodi zilizokuwa zinamkabili.

Katika shtaka la nne,  ilidaiwa kuwa Februari 14,mwaka huu mtaa wa Haile Selasie karibu na Merry Brown, Wilaya ya Kinondoni alishawishi rushwa ya USD 20,000 kutoka kwa Nallavan Vall kama kishawishi cha kuharibu ushahidi uliokuwa chini ya uchunguzi wake dhidi ya kukwepa kodi.

 Februari 10, mwaka huu eneo la  Sabasaba mshtakiwa akiwa mwajiriwa kama Mchunguzi Mkuu wa Takukuru, alipokea Dola za Marekani 20,000 wakati akijua ni zao la kutakatisha na zimetokana na rushwa.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Februari 19, mwaka huu eneo la Village Super Market katika dula la kubadilishia fedha za kigeni la Electron, mshtakiwa alibadilisha sehemu ya USD 7,000 (alipata Sh milioni 16.1) kati ya 20,000 huku akijua ni zao la kosa la rushwa.

Katika shtaka la saba, ilidaiwa kuwa Februari 19, mwaka huu eneo la Chamazi Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam mshtakiwa alinunua ardhi eneo ambalo halijapimwa lenye thamani ya Sh milioni 15.8 huku akijua fedha hizo ni za kutakatisha na ni zao la rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...