KAMATI ya Wataalamu wa Nishati katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imependekeza mataifa hayo kuwa na sheria rasmi za kusimamia miradi ya kimkakati katika sekta ya nishati ili kuwa na utoshelevu wa uhakika wa nishati ya umeme kwa ajili mahitaji ya wananchi wake. 

Hayo yamesemwa leo Ijumaa (Februari 28,2020) Jijini Dar es Salaama na Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati,Adam Zuberi wakati akifunga mkutano wa siku nne wa Kamati ya Wataalamu wa Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichoanza tarehe 24-28 Februari mwaka huu. 

Alisema katika kikao hicho, wajumbe hao walitoa mapendekezo mbalimbali yanayotarajiwa kujadiliwa kwa pamoja katika kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo kinachotarajiwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu, ambapo moja ya mapendekezo yaliyokubaliwa na wataalamu hao ni pamoja na kuweka sheria rasmi ya kusimamia taasisi za kimkakati katika sekta ya nishati ndani ya SADC. 

‘’Katika SADC tuna miradi mikubwa ya kimkakati ambayo sasa tumekubaliana iende mbele zaidi kwa Mawaziri ikiwemo kusaini MOU (mkataba wa makubaliano) ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo inaweza kufanya kazi’’ alisema Zuberi. 

Aliongeza kuwa miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotarajiwa kupewa kipaumbele katika uendelezaji wake ni pamoja na Uimarishaji wa Kituo cha Umahiri katika Uendelezaji wa Nishati Jadidifu na Matumizi Bora ya Nishati (SACREEE) pamoja na kuratibu utoaji wa mafunzo kwa wataalamu kuhusu nishati ya umeme. 

Alibainisha mradi mwingine ni pamoja na uendelezaji wa kituo cha umahiri cha kafue uliopo nchini Zambia, ambacho kitatumika kama chombo rasmi cha Jumuiya hiyo kitakachotumika kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya nishati katika jumuiya hiyo. 

Kwa mujibu wa Zuberi alisema mapendekezo mengine yaliyojadiliwa kwa mapana na wataalamu hao SADC ni makubaliano ya pamoja katika kuwa na miradi ya pamoja ya kimkakati kuunganisha nchi moja na nyingine ili kuhakikisha kuwa nchi za SADC zinakuwa na nishati ya umeme wa uhakika. 

Kwa mujibu wa Zuberi alisema mapendekezo mengine yaliyotolewa ni pamoja na kuwa na mpango kabambe wa matumizi ya gesi asilia (2012-2027)ambapo kwa sasa tayari mshauri mwelekezi tayari amepatikana kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo mwezi Agosti mwaka jana.
  Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia mkutano huo uliomalizika leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
  Kamishina wa Mafuta na Gesi kutoka Wazira ya Nishati, Bw.Adam Zuberi akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mara baada ya Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kumalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania. Picha na na Michuzi JR.
 Kamishina wa Mafuta na Gesi kutoka Wazira ya Nishati, Bw.Adam Zuberi akiendesha Mkutano wa Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania
 Mkurugenzi wa Miundombinu Sekritarieti ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Mapolao Rosemary Makoena akifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka nchi wanachama ulimalizika leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
 
 Wataalam wa Sekta ya Nishati kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wakifuatilia mkutano huo uliomalizika leo Februari 28, 2020 JNICC Jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
 Mwakilishi kutoka Angola akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mwakilishi kutoka Zimbabwe akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwakilishi kutoka Tanzania akifuatilia Mkutano wa Wataalam wa Nishati kutoka Nchi za SADC uliomalizika leo katika Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam, Tanzania.Picha Idara ya Habari-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...