Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWIGIZAJI mdogo kabisa Nikita Pearl Waligwa aliyeng'ara katika filamu ya "Queen of Katwe" amefariki dunia akiwa na miaka 15 na kwa mujibu w vyombo vya habari nchini Uganda vimeripoti kuwa Nikita alipata tatizo la uvimbe kwenye ubongo.

Katika Filamu hiyo iliyotoka mwaka 2016 inamwelezea mtu mwenye maarifa kutoka maeneo ya makazi duni nchini Uganda aliyekuwa anacheza mchezo wa Chess.

Filamu hiyo ambayo ni kisa cha kweli Cha Phiona Mutesi ambaye alianza kucheza chess akiwa na miaka 9 pekee ambapo licha ya kutosoma alishiriki mashindano hayo hadi kufikia ngazi ya kitaifa.

Katika Filamu hiyo iliyobeba kisa cha Phiona Lupita Nyon'go aliigiza kama mama yake, Oyelowo David aliigiza kama.mwalimu wa Chess huku Nikita akiigiza kama Gloria rafiki wa Phiona aliyemwelezea Sheria za mchezo huo.

Imeelezwa kuwa mwaka 2016 alipatikana na uvimbe katika ubongo ambapo kwa mujibu wa daktari nchini humo amesema kuwa hawakua na vifaa kwa ajili ya matibabu ya Nikita huku msimamizi wa Filamu ya Queen of Katwe akieleza kuwa  fedha zilichangishwa na alipelekwa India kwa matibabu na aliendelea vizuri kwa mwaka 2017 lakini mwaka jana alipata uvimbe mwingine uliompelekea umati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...