Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

PETER Muiya muumini wa kanisa katoliki la Mtakatifu James lililopo Muranga nchini Kenya amewekwa chini ya ulinzi kwa tuhuma za wizi wa sadaka katika kanisa hilo, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.


Imeelezwa kuwa kanisa hilo lilitazama video zilizofichwa (CCTV) baada ya kugundua kuwa fedha zimepotea kutoka kasha maalumu zilipohifadhiwa na kugundua kuwa Peter alitengeneza njia kanisani humo na kutumia waya mwembamba kutoa fedha hizo kutoka katika kasha.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na uongozi wa kanisa imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa siku ya Alhamisi February 13 na atashtakiwa kwa wizi.

Makasisi wamepata wakati mgumu sana kuamini kuwa Muiya alikuwa mwizi kwa kuwa alikua muumini na mhudhuriaji mzuri wa ibada.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo aliigiza akisali mara baada ya ibada kuisha na waumini wengine kutawanyika kurudi majumbani na kutumia mwanya huo kuiba matoleo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...