Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI (E) Gerald Mweli ameridhishwa na ujenzi wa mabweni mawili  katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani iliyopo Jijini Dar es salaam.

Mweli ameonyesha kufurahishwa na hali hiyo alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa mabweni hayo pamoja na miundombinu mingine inayoendelea kukarabatiwa katika shule hiyo.

Akizungumza katika ziara hiyo Mweli amesema mabweni  hayo mawili yatakua na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kila moja hivyo wanafunzi 160 wakike watapata fursa ya kukaa katika mabweni hayo.

Fedha hizi zimetolewa maalum na Serikali kwa ajili ya kuwasaidia na kuwajali watoto wa kike waweze kusoma kwa amani na wapate mazingira bora ya kujifunzia  katika kipindi chote cha masomo yao na kuwaondolea vikwazo vinavyoweza kuathiri kumaliza masomo yao kwa usalama.

Ameongeza kuwa miundombinu ya shule hii ilikua imechakaa sana kwa sababu shule hii imejengwa mwaka 1928 na ni maalum kwa watoto wa kike pamoja n wale wenye mahitaji maalum wote wanasoma katika shule hii.

Mweli amesema kuwa zaidi na ujenzi wa mabweni hayo Mhe. Rais John Pombe Magufuli alitoa Sh milioni 90 kwa ajili ya ukarabati wa miundombunu ya shule hiyo hivyo kwa kiasi  kikubwa zimesaidia kuifanya shule hiyo kuwa katoka hali nzuri.

Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika ndani ya mwezi mmoja na ahakikishe kuwa mabweni hayo yanapata vitanda vyote kwa ajili ya wanafunzi waliochaguliwa katika shule hiyo kuyatumia.

Pia amewataka Walimu wa shule hiyo kuongeza juhudi katika kufundisha na kusimamia wanafunzi ili waweze kuondoa zero  na daraja la nne kabisa na kurudisha hadhi ya shule hiyo.

Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu Sekondari OR-TAMISEMI kuhakilisha analeta vitabu vya kutosha vya kujifunzia katola shule hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Gerald Mweli (mwenye tai nyekundu) akiwa kwenye ukaguzi wa Shule ya Sekondari Jangwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...