Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka wananchi kunywa maziwa kwa wingi ili kuvutia wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya maziwa nchini

Naibu Waziri Ulega amesema hayo leo (23.02.2020) wakati wa mbio za kuhamasisha unywaji wa maziwa zilizofanyika viwanja vya The Greens Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mhe. Ulega amesema kwa sasa kiwango cha unywaji maziwa kwa mtu kwa mwaka nchi Tanzania ni wastani wa lita 47 pekee.Kiwango hiki ni kidogo kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza lita 200 kwa mtu kwa mwaka.

“Ili kuongeza unywaji huu wa maziwa wananchi hawana budi kunywa maziwa kwa wingi hali itakayopelekea wawekezaji kuwekeza kwenye viwanda vya kusindika maziwa.” Amesisitiza Mhe. Ulega

Aidha ametoa wito kwa Kampuni ya maziwa ya Woodland kutumia maziwa ya wafugaji nchini ili kuchochea ongezeko la uzalishaji wa maziwa sambamba na kujenga vituo vya kukusanyia maziwa ili kuweka misingi mizuri ya kukusanya maziwa kwa wafugaji.

Mhe. Ulega amesema kwa sasa wafugaji wengi wamekosa soko la maziwa jambo linalopelekea maziwa mengi kumwagwa.

Ameitaka kampuni ya Wooland inayotengeneza maziwa ya First Choice kuangalia namna bora ya kuwekeza hapa nchini ili kusindika maziwa kwa kutumia maziwa ya wazawa na hivyo kuongeza uzalishaji wa maziwa na kufikia azma ya serikali ya ujenzi wa viwanda nchini.

Sambamba na hilo Mhe.Ulega ametoa pongezi kwa Bodi ya Maziwa kwa juhudi kubwa wanazofanya za kuhamasisha unywaji wa maziwa nchini.

Mhe. Ulega amesema Bodi ya Maziwa haina budi kushirikiana kwa Karibu na wadau ili kuweza kubaini Changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi ili kuchochea uwekezaji utakaopelekea maendeleo ya tasnia ya maziwa nchini.

Aidha, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt. Sophia Mlote amesema bodi ipo tayari kushirikiana na wadau wote wa maziwa nchini watakaoonyesha nia ya kutaka kuchochea uzalishaji wa maziwa nchini.

Dkt. Mlote ameipongeza kampuni ya Woodland kwa kuonyesha nia ya kuchochea maendeleo ya sekta ya maziwa hapa nchini kwa kuhamasisha unywaji wa maziwa kwa wananchi.

Kwa ubande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Tanga Fresh,Ally Sechonge amesema kuwa maziwa ni mhimu na ni chanzo mhimu katika kuongeza kipato, pia ukinywa maziwa unakuwa na afya njema.

amesema zao pekee linaloweza kuvunwa kwa mwaka mzima ni maziwa ambayo unaweza kuvunwa kwa kila siku iendayo kwa Mungu ukilinganisha na mazao mengine yote.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mbio za kuhamasisha unywaji wa maziwa zilizofanyika katika vya viwanja vya Farasi Oysterbay leo jijini Dar es salaam. ambapo amewataka wananchi kunywa maziwa kwa wingi ili kuvutia wawekezaji kuwekeza kwenye sekta ya maziwa nchini.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Picha ya pamoja
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (katikati)akifanya mazoezi wakati wa mbio za kuhamasisha unywaji wa maziwa zilizofanyika viwanja vya viwanja vya Farasi Oysterbay leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...